Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Hizi habari za soft drinks na juisi tumeiga tu kwa wazungu lakini watu weusi hazitufai kabisa.
Kwanza metabolic rate ya mzungu ipo juu kuliko ya mtu mweusi. Pengine sababu ni wao kuishi maeneo ya baridi. Hivyo mzungu anachakata chakula haraka kuliko mtu mweusi.
Pili magonjwa yatokanayo na ulaji m-baya na maisha ya bila mazoezi huwaathiri sana watu weusi kuliko wazungu. Hatari ya muafrika kupata kisukari aina ya pili ni mara mbili ya mzungu. Pia magonjwa kama High blood pressure yanawapata sana watu weusi kuliko wazungu. Na hata madhara yake huwa makubwa zaidi kwa weusi kuliko wazungu.
Sasa, pamoja na hatari hii, bado tunakula vitu sawa. Coca cola zile zile, pepsi zilezile, juisi na vyakula vingine, kitimoto na nyama ya kopo, na siagi na mikate vilevile. Hii ni kujihatarisha. Fikiria hapo. Hatari ya kupata kisukari aina ya pili kwa mtu mweusi ni mara mbili ya mzungu.
Kihistoria, inaonyesha binadamu tunapenda sana vyakula vya sukari na mafuta sababu vilikuwa adimu sana miaka hiyo tunakimbiza wanyama porini. Hatukuumbwa kula sukari na mafuta mengi kama tunayokula leo.
Napendekeza kuwe na onyo kwenye juisi na softdrinks zote. Zikisema unywaji kupita kiasi ni hatari kwa afya. Hata vyakula vya mafuta mengi viwekewe maonyo hayo. Tusiige ulaji wa wazungu, tupo tofauti kulingana na mazingira yetu. Tunachofanya kwenye chakula, ni sawa na mzungu amuige mtu mweusi kujianika juani.