MALKIA WA TABASAMU
Member
- May 23, 2024
- 15
- 43
KATIKATI nguvu ya KIAPO.
Muuguzi aliyesalia nami katika chumba kile cha matibabu, haraka sana alinikimbilia na kuniita jina langu. Alitabasamu na kuniambia "karibu" binafsi nilizidisha mshangao,
"Dakitari wako anakuja sasa hivi, naomba usijitikise mwili tafadhali" machozi yalianza kunimiminika.
"Muda wote unalia, tangu uko kwenye 'koma' wewe machozi yakutoka tu, jipe moyo dada, majaribu kaumbiwa mwanadamu" muuguzi aliongea.
Binafsi uchungu au maumivu makali huuzuia sana ulimi wangu. Dakitari aliingia, alikuwa kavalia barakoa na glavu mikononi, alionekana ima katoka kwenye chumba cha upasuaji au katoka kudunga mtu sindano. Alivua glavu na kuziweka kwenye kifaa cha kutunzia uchafu. Alichukua glavu nyingine kwenye kikasha juu ya meza na kuzivaa, hakunijia moja kwa moja, alianza kwa kunikagua. Kuna mahali aligusa maumivu yake sikuweza kuyavumilia, nilipiga ukunga kama mtoto mdogo. Muuguzi aliniwahi na kuzuia mapaja yangu yasirukeruke. Kwakufanya hivyo, nilichokihisi kikaanza kujithibitisha. Sauti ya mwisho wakati wa ajali ikajirudia akilini. Ni kama yule kaka alikuwa ndani ya chumba kile na kwa makusudi akaniongelea sikioni.
"Hapa tupate msumeno tukate vyuma vilivyofanyika kizuizi, tofauti na hapo akatwe sehemu ya chini ya mwili wake kuokoa maisha yake"
"Hapanaaaa! Msinikate miguu yangu! Nawaomba sana msinikate miguu yangu" niliongea kwa uchungu mkali. Nilitapatapa kiasi cha kumshinda nguvu yule muuguzi. "Tabita, naomba utulie, una majeraha makubwa sana na yote bado hayajafunga vizuri" dakitari aliongea kwa upole na msisitizo. Machozi hayakuacha kunichuruzika. Nililia kiutu uzima. Muuguzi alitokwa na machozi ambayo mimi niliyaona, ila alijitahidi sana mkubwa wake wa kazi asiyaone. Aliingia muuguzi mwingine. Alimuita dakitari na kuteta naye jambo. Nilisikia tu, "usimhabarishe yoyote hadi tuwe na uhakika" alirejea na kumwambia muuguzi aandae mazingira ya 'dressing'.
Bado sikuwa katika hali ya kawaida. Sikujimudu kihisia wala kimhemko. Mashaka na hofu vilinitawala, kuna utofauti wa kimaumbile niliuhisi tangu niliporejelewa na fahamu; nikajifariji tu kuwa ni ndoto mbaya itakayopotelea mbali nikiamka. Vifaa vilifika, kabla ya chochote kutendeka dakitari alinisogelea.
"Beautiful Tabita, how are you doing? Aliuliza dakitari. Sikuwa na neno, niliibetua midomo na kuchezesha kichwa ishara ya kuwa sijui naendeleaje. Aliniomba niinyanyue mikono yangu, nilifurahi kuona yenyewe iko sawa. Ilikuwa na vijikovu vidogo vidogo vipya. Sikuwa hata na nguvu ya kuviongelea. Ni kama niling'atwa ulimi, maswali yaliyonijaa hadi pomoni, niliyaacha kama vile kuna mahali nitayatumia baadae.
"Pole kwa ajali. Leo ni siku ya hamsini na moja tangu ufiķwe na jaribu hilo, na ni siku ya arobaini na mbili tangu uletwe hapa hospitali kwetu. Tunamtukuza Mungu. Mengi tuliyoyahofia yamekarabatika bila ya sisi kugharamika. Utakuwa na vipimo vya mwisho, vitakavyotupa tathmini sahihi ya maendeleo yako. Hongera kwa kuwa jasiri" nilimsikiliza dakitari ila kusema kweli nguvu ya kujibu sikuwa nayo kabisa. "Kuna taarifa mbili natakiwa kukupa. Kila moja imekaa upande wa pili kihisia kinyume na nyenzake" dakitari alinitazama kwa sekunde chache na kumeza fundo nono la mate.
"Ni masikitiko yangu kama dakitari niliyekabidhiwa wewe kama jukumu kukupasha habari hii. Nilijaribu kuomba mtu mwingine wa kuikupatia bila ya yeye kuumizwa nayo ila sikupata msaada. Najisikia vibaya kama binadamu, ila kazi ya Mungu haichunguziki" dakitari alizunguka sana, kuna namna nilikerwa na hilo ila sikutaka kukurupuka. Nilijituliza nione tamati. Kwanza sikuwa hata kwenye mpangilio wowote wa hisia. Ni kama nilikuwa nimechanganyikiwa tu.
"Umepoteza uwezo wako wa kutembea" aliongea dakitari.
"Nitatembea tena? Nilimuuliza.
"Hapana Tabita, hutoweza kutembea tena"
"Kwanini dakta?
"Nachelea kusema, umepoteza miguu yako yote miwili" Dakitari aliongea hali wajihi wake ukiutazama ukuta......
KARIBU USOME RIWAYA HII MPYA KWA MFUMO WA NAKALA LAINI.... KWA KULIPIA ELFU 3 TU KWA LEO. Tarehe 1/7/2024...
BAADA YA LEO SOFTCOPY ITAKUWA SHILINGI ELFU 7..
LIPIA 0742 6301 41 Jina Felix Kyando.
Nitumie uthibitisho watsup namba hiyohiyo, nami nikutumie PDF yako swafi kabisa.
Nimeandika usome. Hiki ni kipande kidogo sana kìlichopo katikati ya mkasa wa maisha ya Tabita Komba.