SOKA LA AFRICA KILA KITU KIPO NJE YA UWANJA

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
fainali mkondo wa kwanza nyumbani kwa WYDAD

1.ESPERANCE wanapata goli

2. Beki wa WYDAD anapata kadi nyekundu baada ya kupewa njano mbili

3.WYDAD wanasawazisha goli , goli linakataliwa baada ya refa kuangalia VAR

4.WYDAD wananyimwa penalti baada ya beki kuunawa Mpira ukielekea nyavuni refa anaangalia VAR na kukataa tuta

5.WYDAD wakiwa pungufu wanasawazisha goli[emoji460][emoji460][emoji460]

6.mechi inaisha 1-1 pale MOROCCO [emoji810][emoji810][emoji810]

7.refa aliechezesha mechi ya fainali ya kwanza anafungiwa miezi 6 kutokakana na maamuzi mabovu kwenye mechi hio

8.mechi ya marejeano ( fainali ya pili) nyumbani kwa ESPERANCE

9.ESPERANCE wanapata goli la kutangulia

10.WYDAD wanachomoa na goli halali linakataliwa kwa madai ya kua MFUNGAJI alikua OFFSIDE

11.WYDAD wanamlalamikia mwamuzi akaangalie VAR lakini mwamuzi anagoma

12.WYDAD wanagoma kucheza mpakaa VAR iangaliwe

13.VAR inagundulika kua ni mbovu na haifanyai kazi

14.RAIS wa CAF anaingia mpaka uwanjani kuomba mechi iendelee bila VAR lakini WYDAD wanagoma wakidai wanaonewa wazi wazi

15.kapteni wa ESPERANCE anadai mwamuzi aliwaambia kabla ya mechi VAR ni mbovu lakini kapteni mwenzie wa WYDAD hakuelewa lugha ya mwamuzi

16.ESPERANCE anakabidhiwa kombe kwa mara ya pili baada ya mechi kuvunjika.

THIS IS AFRICA[emoji276][emoji276]
 
Aibu tupu kwa soka la Afrika, na kwa CAF, hasa rais wake. Angechukua tahadhari baada ya figisu za mechi ya kwanza.
 
Mimi unadhani kuna haja tuanzishe mpira wa kucheza mdomoni,wanakaa watu wawili wanaanza cheza mpira kwa Maneno yao....
Hahahaha hata huo wazungu watakuja kutushinda tuu sisi hakuna kitu tubaweza yani hata vya kijinga
 
Dawa yake ichezwe mechi moja tu ya fainali na iwe neutral ground kama ulaya
Itakuja changamoto ya Uwanja sasa labda wafanye kama Uefa kwamba wautenge Uwanja kabla ya kufika fainali japo Kiafrika Afrika si ajabu game ikachezwa pasi kuwa na washabiki Uwanjani kutokana na majografia na hata gharama pia.
 
Dawa yake ichezwe mechi moja tu ya fainali na iwe neutral ground kama ulaya
Hata huko ulaya hakuna natura ground kumbuka mechi ya Bayern na Chelsea mwaka 2012 kama ilichezwa natural ground au msimu huu atletico wangefika final mechi ingekuwa kwenye natural ground?
 
Hata huko ulaya hakuna natura ground kumbuka mechi ya Bayern na Chelsea mwaka 2012 kama ilichezwa natural ground au msimu huu atletico wangefika final mechi ingekuwa kwenye natural ground?
Neutral ground ni fikra tu mkuu lkn kikubwa ni kwamba uwanja utangazwe kabla hata ya kufika fainal. Kama timu ya nchi husika ikifika fainal ni faida kwa timu husika lkn kikubwa pale ule uwanja unakuwa chini ya shirikisho na siyo kilabu. Hata ikitokea neutral ground ni kwa mkapa. Then moja ya timu za tff zikafika final ule uwanja wakushughulika nao kwa kila kitu ni caf na siyo tff club.

I stand to be corrected
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…