Soka la bongo linayumbishwa na uelewa mdogo

Soka la bongo linayumbishwa na uelewa mdogo

Mohamed Mbelwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
507
Reaction score
272
YANGA VS AZAM. Yanga alishinda goli 1-0 dhidi ya Azam pamoja na mapungufu ya referee kutoa maamuzi lakini hukusikia kocha, viongozi wala mashabiki wa Azam wakisema referee kawabeba Yanga, hawakusema kutokana na ukomavu na uelewa wao ktk soka wakitambua wazi refa pia ni Binadamu hivyo km Binadamu kuna makosa mengne hufanya kwa bahati mbaya.

Lakini upande wa pili mchezo huo huo Azam angeshinda na mapungufu yale ya refa tungesikia maneno refa alikuja na matokeo yake mfukoni kitu ambacho si lugha ya kimchezo tujifunze kukubali matokeo pale tunaposhindwa na kuwapongeza washindi.

KAGERA SUGAR 2-1.Tunaona pamoja na ratiba ngumu waliokuwa nayo Simba ata baada yakupoteza mwalimu alipohojiwa alikiri timu yake haikicheza vizuri na anajua alikosea wapi atafanyia marekebisho mapungufu yale na kuwapongeza KAGERA kwa ushindi, ile ndo lugha ya kimchezo.

PENALTY. Kwenye mpira wa miguu sheria haijaweka kiwango (idadi) ya penalty ndan ya dakika 90 bali adhabu ya penalty itatolewa kwa mujibu wa kosa pacpo kujali idadi ya penalty wala muda wa mchezo mathalani kosa limetendeka ndani ya eneo la 18 na refa kajilidhisha kuna kosa basi penalty itatengwa ata kama zimeshapigwa 5 na bado kosa limetendeka ndani ya 18 itatengwa tena kwaiyo mashabiki lazima mlielewe hilo mcpende kulaumu bila kujua taratibu inasemaje.

MUDA WA NYONGEZA. Kwa kawaida inatafsilika kuwa mchezaji tofauti na kipa ana dk 1 ya matibabu ndani ya uwanja kwaiyo inapotokea wametibiwa wa3 inamaana kuna dk 3 zimepotea,, sasa kwa kutojua au kwa makusudi wachezaji wetu wamekuwa wakipoteza muda kwa mtindo huo bila kujua kuwa muda huo unahifadhiwa ama kujiangusha kwa makusudi na inapotokea muda kuongezwa zaid ya matarajio yao wao hulaumu bila kukumbuka muda waliopoteza na hili lilitokea IRINGA mchezo wa LIPULI VS YANGA mchezo ukachezwa dk 99, pia mchezo kati ya SIMBA VS JKT TANZANIA mchezo ukachezwa dk 97 hii yote ni kutoelewa kwa wachezaji wetu, wenzetu wana mbinu zao zakupoteza muda eidha wauchezee mpira kwenye eneo lao zaidi au kwenye eneo la kona ya mpinzan co kujiangusha ovyo uwanjani.

Tuepuke MIHEMKO na unazi kwenye SOKA letu ligi itapendeza aliyeshinda apongezwe na aliyeshindwa afanyie marekebisho mapungufu yake tusipende kulaumu sana soka la mdomoni halitatusaidia.
 
Waambie hao mashabiki maandazi ambao wao refa anakuwa mbaya Simba akishinda ila akifungwa refa anakuwa supa brand!pia wao wakifungwa refa kimeo wakishinda anakuwa supa jiniaz!yaani hadi jamaa wanaongoza ligi lakini ukiwaangalia huku mtaani wamekaakaa Kama wafiwa jinsi nyuso zao zinavyojaa huzuni Kila mnyama anapogawa dozi!
 
Ha ha haaa, wanawake wa Pwani huwa waoga kuwaambia waume zao au adui zao yanayowasibu mioyoni hivyo huzunguka kwa mafumbo, kuvaa khanga za jumbe nk.

A real man calls spade for spade!
Ebu watajeni hao wanaowasumbua mioyoni mwenu...
 
Hii ni mbinu ya Yanga kutuathiri kisaikolojia wala hakuna ukweli wowote,ingekuwa nia ya Yanga ni kulaumu kiwango kibovu cha marefa wangeleta na reference ya matukio kama haya yanayotokea ktk mechi zingine zikiwamo zao wenyewe wangekemea pia

Bahati mbaya wametukuta Simba tuko imara kisaikolojia.

Ingawaje mbinu yao ya kupiga mayowe inaathiri uwezo wa marefa kuamua vizuri dhidi ya Simba wakihofia wataonekana wanapendelea Simba ndio maana utaona Jana Simba kanyimwa penati.Sasa hivi ili Simba ipewe penati labda mchezaji wetu aangushwe eneo LA penati,mchezaji pinzani achukue panga amkate kichwa mchezaji huyo wa Simba amtenganishe na kiwiliwili ndio refa atalazimika kutoa Penati kwa Simba.

Lakini tutapambana hadi mwisho.
 
Wapuuzi wachache hawawezi kutuletea shida. Jana HB amejidondosha weeee,ila alivyopigwa kitu akiri zikarudi hakujiangusha tena.

Halafu Simba ni timu kubwa lazima marefa wapambane kulinda mastaa wetu wenye thamani kubwa kiwango kikubwa.
 

Kuna watu humu hata hawaangalii Moira,wanasubiri Simba ifunge waanze mikelele
 
Kweli kipato huleta majivuno! Simba mmesahau kipindi kile mnakesha mkilalamikia marefa na kina Malinzi! Ni nani aliwahi kwenda kuongea na waandishi wa habari na TV kama sio simba? Nani waliokwenda FIFA kulalamika kama sio simba? Mnataka mlalamike nyie tu! Hakuna watu walalamishi katika nchi hii kama simba! Sema vihela vya Mo ndio vimewasaulisha!
 
roho yangu hinauma nikiona kijana wa kitanzania anaongelea soka la tanganyika
 
Ukweli mtupu.

Naunga mkono hoja mkuu.
 
Back
Top Bottom