Soka linajitosheleza, halimhitaji mkuu wa mkoa Dar au Rais na hata siasa kwa ujumla ili kupata mashabiki

mkulimamiwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2025
Posts
2,591
Reaction score
5,315
Soka na CCM ni mbingu na aridhi

Wakati mashabiki wa CCM wakihitaji kupelekewa maloli ya bule vijijni kimokela huko na mbagala kwa msewe, Boko na Magomeni mapipa ili kuja kujaza viwanja vya Jangwani, Mashabiki wa soka hutoka Mwanza, Arusha, mbeya, kigoma, Kenya, Congo na hata ulaya kwa pesa zao na kuja Dar kujaza uwanja wa Mkapa

Kitendo Cha CCM kulifanya soka kuwa sehemu ya Siasa ni matusi kwa wapenda soka

CCM mnakuwa kama watu washamba msio na aibu kabisa

Kufuzu fainali kwa Serengeti boys under 17, sio jitihada za siasa, sio jitihada za mkuu wa mkoa wa Dar, na siyo jitihada za Rais

Soka liwaheshimu vijana wetu,

Sehemu salama ambayo ninaamini Haina itikadi, ni soka pekee, sasa hii ya Mama Mia moja ashukuriwe, inatoka wapi?

CCM mnapenda vitu vizuri utadhani mnajua kuvitengeneza

Niwakumbushe, CCM hajawahi kutengeneza kitu kizuri kwenye nchi hii tukajivunia

Kila kilichoanzishwa na CCM kina ila hata kikikamilka, bado hakitadumu

MAma Mia asifiwe na au alaumiwe, ni kwenye siasa huko na si kwenye soka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…