Diamond Platnumz alipokutana na Cloutas Chama na Kenedy Musonda katika uwanja wa ndege Julius Nyerere International Airport, ilikuwa ni tukio la kufurahisha, hususan kwa mashabiki wa soka na muziki. Wakati Diamond akielekea Zimbabwe kwa ajili ya shoo, wachezaji hao walikuwa wakielekea Zambia kujiunga na timu ya taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu AFCON na timu ya Taifa Chad.