SoC02 Soka na Uchumi wetu

SoC02 Soka na Uchumi wetu

Stories of Change - 2022 Competition

Yazidu Hamza Bitika

New Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
4
Reaction score
1
SOKA NA UCHUMI WA TANZANIA.

Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania... Awali ya yote nipende kukushukuru wewe ndugu yangu, uliyetega jicho na kufungua ubongo wako kwa umakini ili kujifunza juu ya mada hii.

Tanzania ni katika mataifa yanayokabiliana na tatizo Kubwa la ukosefu wa ajira, na tatizo hili linazidi kukua siku hadi siku kwasababu idadi ya Watu inazidi kuongezeka siku hadi siku, sababu kubwa ya hili ni mfumo duni wa maisha unaowajengea vijana taswira duni katika vichwa vyao, soka ni katika nyanja zinazoweza kutukwamua kwa kiasi Fulani na tukaweza kupunguza tatizo hili la ajira kwa vijana.

Naamini Watanzania wote tunakubaliana kuwa soka ni mchezo pendwa zaidi katika taifa hili kuliko michezo mingine, ni mchezo wenye wafuasi wengi zaidi kuliko mchezo wowote ndani ya taifa hili, lakini haitoshi taifa hili Lina vipaji vingi vya soka kuliko tasnia nyingine yeyote. Hivyo basi kama hali ya soka Tanzania iko hivyo tukae kutizama tu? au tufanye Nini?

Taifa la Brazil ni walimaji wazuri wa miwa lakini walipogundua kuwa ndani yao Kuna madini ya soka ambayo yanaweza kukuza uchumi wa Taifa lao waliyachimba na kuyaingiza sokoni na kusaidia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa Taifa hilo. Marekani ni Taifa lenye ubobezi mkubwa katika kilimo Cha mahindi lakini walikuja kuigundua tunu ya mpira wa kikapu katika nafsi zao. Hadi mpira wa kikapu unawaingizia marundo ya fedha.

Kuna taifa kinaitwa Uingereza wao hawana vipaji vikubwa sana vya mpira lakini wanaupenda na watu wa taifa hilo wanaupenda, taifa likawekeza katika ligi na kwasababu watu wanapenda mpira, waliitikia na kuingia matrilioni ya fedha kwa kupitia kitu kidogo tu, hadhi. Ukienda India wao walijitathmini na kugundua ubora wao uko wapi, wakajikita kwenye filamu na wakafanya vizuri, duniani hapa hakuna taifa lisiloijua India katika ulimwengu huo.

Hata Afrika hapa ukitazama mataifa mengi ya Afrika magharibi kama Senegali, Nigeria, Burkina Faso, Cameroon na mengine wamewekeza kwenye soka na vijana wengi wa mataifa hayo mpira ni ajira yao, na ndio maana unawaona wametanda ndani na hata nje ya Afrika kutafuta ugali wao. Ukiangalia South Africa ni taifa linalofanya vizuri katika ligi ya soka, na ni kwasababu wamewekeza, ndio maana ligi yao inaingiza mapato mengi, ndio maana waswahili wanasema, unavyotoa zaidi ndivyo utakavyoingiza.

Haya sasa, tunarudi Tanzania, sisi tunakitu gani?, Ukiitazama Tanzania ni nchi ambayo watu wake wamejikita kwenye kufanya kila kitu, kwasababu watu wake ni wafuata upepo, wakisikia Leo muziki umetema, utawaona wote wanazama huko. Kesho wakisikia Kunasoka la ufukweni wataenda huko, si mbaya sana, lakini nadhani kutambua ubora wako ulipo ni jambo muhimu sana katika maendeleo, hata katika madarasa ya uchumi utasikia sana hii kauli ya kuwekeza nguvu kwenye kitu kimoja, na hii inasaidia sana.

Mimi nadhani Tanzania kwenye upande wa soka tuko vizuri sana, kwanza tunalo soko la mpira nikimaanisha washabiki wa mpira, si wanaume si wanawake, si vijana si wazee, si vjijini si mjini, kila Kona ya taifa hili imejaa washabiki wa soka, ambao hao ndio mtaji wenyewe nasema hivyo kwasababu hao ndio hulipa fedha za viingilio, hao ndio wananunua jezi, hao ndio wanalipia visimbuzi na kuingiza mapato mengi.

Si hivyo tu bali hata katika vipaji, mimi nadhani mojawapo mwa chanzo kikubwa cha uchumi ni kile kinachozalisha ajira nyingi. Soka linavipaji vingi sana Tanzania hii, tena vikubwa na vinavyouzika, tazama jioni na asubuhi vijana wangapi wapo viwanjani, utakuja kugundua kunawatu wananyimwa na mfumo tu, si kitu kingine.

Hebu tuwekeze kwenye vipaji vya soka, alafu tuwatume vijana wakatande huko nje, vijana wajae kwenye ligi za ndani na nje, tuwafungulie milango, ili tupunguze idadi ya vijana watakaoilalamikia serikali kuhusu ajira, pili uwe ni mwanzo Bora wa timu ya taifa yenye ushindani na tatu tuwe na ligi Kubwa zaidi Afrika na inayofuatiliwa zaidi na Hilo linawezekana.

Hebu nizungumzie kwa kifupi kuhusu uchumi wa soka katika kuandaa michuano mbalimbali ya kimataifa, kama Kuna fursa kubwa ya kufungua uchumi wa nchi basi moka wapo ni kuandaa hii michuano ya kimataifa kama kombe la dunia na kadhalika, na shida inapokuja ni kwenye maono ya viongozi wetu, Kuna Rais mmoja aliwahi kupita kwenye taifa hili alijikita sana kwenye miundombinu watu baadhi walimbeza lakini wakasahau hata kuandaa tu, mashindano ya kimataifa wanaangalia miundombinu uliyonayo, kwamfano Dar es salaam inashindwa kukidhi matakwa ya usafiri ya raia wake, mpaka kunatokea foleni na adha nyingi je, tukiwapa muandae Afkon Afrika yote ikahamia Tanzania tutasafirije kwa uhakika kuwahi mechi?.

Tukitoka kwenye mechi moja ya mchana iliyochezwa kwa mkapa na tunataka kuwahi Chamazi kuangalia mechi nyingine, tutaweza? Ikiwa mechi tu ya Yanga na Simba usafiri unakua tatizo wakati wa kuondoka?, Mimi kama mzalendo na ninatamani siku moja na sisi tuandae mashindano makubwa ambayo yatasaidia kukuza uchumi wa Taifa kwa kiasi kikubwa nashauri serikali ijenge miundombinu ya kutosha hasahasa usafiri, Kuna wafanyabiashara walikua wakifanya biashara zao CCM Kirumba kwenye mechi ya Senegal na Kenya kesho wanataka wawe Dar kuendeleza biashara zao za vyakula na jezi na vuvuzela pakiwa na treni ya kuserereka si watu watawahi, wale washabiki si watatazama mechi zote?.

Mahoteli yatajaza mpaka nyumba za kulala wageni vyakula vitauzwa, utalii utafanyika miundombinu itaboreshwa zaidi kama ya viwanja na kadhalika na faida nyingi Kubwa na hapo ni kwa uchache, nadhani tunaelewa ni vipi soka linaendana na uchumi.

Naomba niwaonyeshe namna Watanzania walivyotayari kuungamkono vitu vyao vya nyumbani, Mbwana Samatta aliposajiliwa katika klabu ya Astonvilla, ukurasa wa timu hiyo wa Instagram ulifurika wafuasi, na hii ilionyesha nguvu ya Watanzania kwa watu wao. Hivyo mimi nadhani soka ni fursa Kubwa sana ya kukuza uchumi wetu na kupunguza tatizo la ajira, soka linaajiri watu wengi sana.

Kila mtu ni shahidi juu ya mapato yanayopatikana katika mechi za Simba na Yanga tu, mamilioni ya pesa huingizwa kama mapato, kama tukiamua kuwekeza kwenye soka inawezekana kuzitengenezea nguvu timu zote, zikawa na washabiki, na ukizingatia Tanzania ipo katika mataifa tisa yatakayochangia ongezeko la watu duniani kufikia mwaka 2050, hivyo washabiki watakuwepo wengi, na tutaingiza mapato ya kutosha kupitia soka.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika
Kazi iendelee.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom