SOKA TANZANIA NA UBOVU WA MIUNDO MBINU.

Joined
Sep 26, 2017
Posts
22
Reaction score
17
Habari ya muda huu wadau wa michezo,
Niende moja kwa moja kwenye mada husika,mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania umekua na unazidi kukua kwa kasi na kupendwa kwa rika zote,pamoja na jinsia zote,hivyo imefanya hata baba wa mpira (Tff) kuwekeza nguvu kwa upande wa wanawake,hongera kwa hilo.Watanzania ni watu wanao penda sanaa huu mchezo kiasi kwamba imekua kama ni sehemu ya maisha yao,na ndio inayo watofautisha na wana Africa mashariki wengi,hasa kwa kupenda ligi ya nyumbani na kuhudhuria viwanjani kwa kiasi fulani cha kuridhisha.
Pamoja na kuwa na mapenzi ya dhati ya huu mchezo miundo mbinu panapochezewa ndio kizungu mkuti,
Umekua wimbo wa miaka nenda rudi kutoka kwa wadau wa huu mchezo kuhusu viwanja ,
Ukiachilia viwanja vichache vilivyo chini ya harmashauri na vile vya baadhi vinavyo milikiwa na chama tawala (ccm) vinahali ya kuridhisha,
Viwanja vingi hasa vinavyo milikiwa na chama tawala (ccm) vimetelekezwa hasa sehemu ya kuchezea imekua kituko kama mazizi ya ngamia au mashamba ya mpunga.ifike mahala hawa wamiliki wajitathimini,kusu utunzaji wa miundo mbinu hii kwa manufaa ya maendeleo ya michezo, kama wameshindwa basi watafute angalau wawekezaji kuviboresha,
Pia maoni yangu kwa Tff wakae chini na hawa wamiliki japo wakodi sehemu za kuchezea (pitch) na wazifanyie marekebisho kama itawezekana,
Mfano viwanjana kama Sokoine ,Nangwanda,majimaji,Mkwakwani,Namfua vipo taabani kwelikweli.
Miundo mbinu iboreshwe kuendana na kasi ya maendeleo ya mchezo wenyewe.
 
Hivyo viwanja ni vya wananchi wote wa Tanzania! Sema tu hicho chama cha ccm kimeshazoea ukwapuaji, kimevikwapua viwanja vyote mchana kweupe bila hata chembe ya aibu, halafu wanakula tu mapato yatokanayo na viingilio huku wakishindwa kuviendeleza.

Bahati mbaya tff yenyewe nayo ni tawi la hiyo ccm! Walitakiwa waje na mkakati wa kujenga viwanja vyao kila mkoa, au kuzihamasisha timu zote za soka kujenga viwanja vyao kama walivyofanya Azam, Gwambina, Jkt Tanzania, nk.
 
Timu zetu nyingi hazina viwanja, zinategemea vya ccm ambavyo ni vibovu
Mpira wetu tunataka ukue kwa bahati tu kitu ambacho sio rahisi kwenye soka
Hongera AZAM FC, GWAMBINA na wote wenye viwanja vyao bora kwa soka
 
Wangejitathimini hata waviboreshe ingekua poa maana wamevisusa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…