Soko huria ndiyo sababu kubwa inayofanya nchi za Kiafrika zisiendelee

Kufunga mikanda hakuna haja, kwanini ufungishe watu wako mikanda? Wakati unaongoza watu kuwapa mafanikio na maisha Bora? Wala soko huria siyo kikwazo maana kama ni kikwazo mbona miundo mbinu ni mipango ya Nchi lakini watu wanakosa barabara? Maji, hospital, mashule nani amewazuia kujenga? Sasa hivyo vitu vidogo vidogo kama nguo watu wakivaa za nje na za hapa shida ipo wapi? Maisha mazuri ndo Mungu anapenda Kila mtu Aishi hivyo vitu vikipatikana kwa wingi ndo watu wataishi kwa kuchagua kipi watapenda kutumia maana dunia ishakuwa kijiji yule atakayetengeneza vilivyobora ndo vitu vyake vitapedwa zaidi.
 
Waafrika hizi sio zama za kulaumu.Ni zama za kutenda,
 
Afrika mashariki, Kenya ipo juu kiuchumi, ukiruhusu soko huria Kenya watazidi kupeta. Mf wembe wa Tz ni 200 na wa Kenya ni 200, ila wa Tz ni butu ninunue upi?
Kwahiyo tutumie vitu vibaya? Soko huria halina shida kikubwa walete wawekezaji wawambie soko lipo na vitu vyetu havina utaalamu Ili waje wawekezaji wenye utaalamu mzuri na wateja wapo wanasubiri vitu vyenye ubora vitakavyopatikana kwa urahisi.
 
Nani amefanya dunia kuwa kijiji? Ni mataifa tajiri baada ya kugundua kuwa makampuni yao yamekuwa na yanaweza kushindana na makampuni mengine duniani. Lakini sisi hapa, kampuni yoyote itakayojaribu kuinuka itakufa. Haitaweza kushindana na mikampuni mikubwa ya matajiri.

China walikataa Google, facebook Amazon na makampuni mengine makubwa kuingia kwao. Lengo ni ili wakuze makampuni yao, wakatoa Baidu, Alibaba, alipay, Wechat nk. Wangeruhusu google, baidu isingeweza kushindana nayo. Marekani leo kaifungia Huawei, lengo siyo usalama bali wasije wakateka soko la 5G wakati makampuni yao hayawezi kushindana.

Sasa basi, usipokuwa na makampuni makubwa ya kulipa kodi, huwezi kuwa na miundombinu. Lazima ulinde viwanda vyako, si vya nguo tu, hata vya vitana na sahani za udongo, na sindano na kila kitu.
Sasa, ukitaka kulinda viwanda vya nguo, au ngozi kwa kupiga marufuku viatu na nguo za mtumba , lazima watu wakubali hali itakavyokuwa.
 
Ni kujinyonyongonyesha tu lakini hakuna anayeshindana na sisi kwa kiwango hicho hata huko china kwani lazima akauze marekani? Mbona anauza Africa sana tu, sisi hatuna vitu Bora vingi vinavyopatikana kwetu na vingine havipo kabisa yaani havizalishwi nchini kwasababu swala la uwekezaji sisi kama hatuna hiyo ajenda Wala mipango kwasababu serikali haijamwaga pesa kwa watu kiasi cha kufanya uwekezaji mkubwa kama viwanda au kupunguza kodi kiasi cha watu wengi wakipata pesa waaznzishe viwanda Ili ajira zipatikane hivyo tatizo siyo soko huria maana mbona Kuna bidhaa za plastic Kuna kiwanda kinatengeza vitu vizuri vinavyokwenda na wakati mbona watu tunakiungisha sana? Akisikia kabati za plastic kutoka china sijui viti na yeye anatengeneza vya kisasa zaidi, sahani, mabakuli, majagi ya kisasa mpaka meza za kulia chakula katoa na zinauzika? hivyo kwasisi Wala soko huria halitukwamishi ila hatuna pesa na pesa za maana haziwafikii wanaohitaji kuwekeza, itokee Waziri wa uwekezaji apewe fungu la mikopo ya viwanda kwa watu wanaotaka kuanzisha viwanda uone hiyo nguvu ya soko huria inayoonekana Ina nguvu itavyopotea, mfano mashindano ya wazo la biashara yanavyotoa watu wengi wakiwa na uhitaji wa mitaji ya kuzalisha bidhaa tofauti tofauti mbona hawaogopi hilo soko huria kutoa kuhitaji mitaji.
 
Marekani walitishia kuzitoa nchi za EA AGOA iwapo wangepiga marufuku mitumba, usiseme hakuna anayeshindana na sisi. Kuna kitu cha maana umeongea, serikali inatakiwa kuwezesha uanzishaji wa viwanda. Sasa ili nchi iwe ya viwanda inahitaji hilo la watu kusaidiwa na serikali kuanzisha viwanda, na serikali kulinda soko la hivyo viwanda hadi vitakapoweza kushindana kwenye soko huria.

Nchi za Africa hazifanyi hata kimoja kati ya hayo.
 
Kama wengine wameweza hatushwindwu
Kuiweza ndiko kunahitaji utayari na kufunga mikanda. Vita ya kiuchumi inapiganwa kwa tariffs, import restrictions nk. Mambo haya yanaweza leta uhaba na mfumuko wa bei. Yanahitaji watu walio tayari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…