Soko la bata maji

Soko la bata maji

Dadii

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2010
Posts
749
Reaction score
1,158
Heshima kwenu wakuu Jamvini.

Mimi ni mfugaji wa bata maji, nilianza si kwa minajli ya biashara ila kama kitoweo nyumbani. Lakini sasa wamekuwa wengi sana kiasi kwamba nashawishika kufuga kibiashara.
Nimejaribu kupita katika nyuzi za humu ndani ila sijapata haswa wapi soko la hawa bata, tafadhari mwenye kufahamu soko lake tujulishane wadau.

Natanguliza shukrani za dhati.
 
humu humu ndani utatupata wateja pia....unawauzaje kwani...pia picha ingefaa mkuu tuwaone
 
humu humu ndani utatupata wateja pia....unawauzaje kwani...pia picha ingefaa mkuu tuwaone

Mkuu picha nitatuma ila kwa wateja wa humu Jamvini ntauza kwa bei Tsh 25,000/= dume na 20,000/= kwa jike.
Karibu mkuu Babeake.
 
Mkuu picha nitatuma ila kwa wateja wa humu Jamvini ntauza kwa bei Tsh 25,000/= dume na 20,000/= kwa jike.
Karibu mkuu Babeake.

Ila ningependa niwe na supply atleast hata wa 5 per day, kwa hiyo nilikuwa nahitaji soko la uhakika zaidi, si unajua transport cost, maana mdau atakumbia nipo Sinza niletee bata mmoja. ukichanganya na nauli faida unakuwa huioni mdaua.
 
Back
Top Bottom