Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Habari wakuu....
Naomba kufahamishwa kuhusu soko la CHEESE kwa hapa Dar es salaam na bei zake,
Pia kwa wanaofahamu njia tofauti tofauti za utengenezaji wa cheese mnakaribishwa!!
"tujifunze kwa maendeleo ya taifa'
Chakula hiki kina wapenzi wachache hapa Dar lakini hii inatokana na wengi kutokukijua kwani kinaliwa zaidi kwenye burger na pizza na wakazi wasio na ushabiki au interest na vitu kama hivyo ni wengi. Cha msingi ni wewe kuitambulisha kwenye soko taratibu na kuongeza uzalishaji kadri demand yake itakavyoongezeka. Njia rahisi ya kuiintroduce ni kwa kutangaza faida yake, utamu wake na jinsi ya kuitumia katika mapishi na nina uhakika wakiijaribu hawataacha. Binafsi naipenda sana cheese ila supermarket wana bei za kukomoana 7000, 10000, 12000 mpaka 20000, si vibaya kukiwa na source/supplier mwingine mwenye price reasonable!