DOKEZO Soko la Kayenze (Magu) limekithiri kwa uchafu, ukihoji wanakwambia “hama soko”, hali iliyopo ni ya hatari

DOKEZO Soko la Kayenze (Magu) limekithiri kwa uchafu, ukihoji wanakwambia “hama soko”, hali iliyopo ni ya hatari

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Katika likizo yangu ya hivi karibuni nikiwa Mwanza, nilitembelea Soko la Kayenze maarufu kwa jina la "Soko la Wakulima," lililopo Wilaya ya Magu, nilishangazwa na hali mbaya ya uchafu iliyokithiri sokoni humo.
IMG_20250108_145812_809.jpg
Soko hilo ambalo linahifadhi meza takriban 2,000 za Wafanyabiashara, limegeuka kuwa kama dampo la taka. Uchafu kutoka kwenye migahawa ya vyakula, hoteli za jirani, na biashara za ndani ya soko unatupwa kiholela sehemu maalum iliyotengwa na wafanyabiashara baada ya kukosa dampo rasmi.

Harufu mbaya isiyovumilika imetawala soko, hali inayowatia hofu Wafanyabiashara na wateja kuhusu afya zao.
IMG_20250108_145812_357.jpg
Ahadi Zisizotimia na Kodi Zinazokusanywa
Wafanyabiashara wa Kayenze wanahisi kusalitiwa, wanadai walihamishwa kutoka maeneo yasiyo rasmi kwa ahadi za kupewa miundombinu bora, lakini hali iliyo mbele yao ni tofauti kabisa.
IMG_20250108_145812_563.jpg
Walipopewa eneo hili miaka miwili iliyopita, walihakikishiwa kuwa wangefanya biashara katika mazingira bora na salama. Hata hivyo, hali ya sasa inaonyesha wazi kwamba ahadi hizi zilikuwa hewa.

Inaelezwa kuwa kila siku wanalipa ushuru wa shilingi 200 kwa kila meza, huku wauza ndizi wakitozwa shilingi 10,000 kwa mwezi kwa usafi na ulinzi.
IMG_20250108_145812_491.jpg
Licha ya makusanyo haya, soko limeendelea kuwa kwenye hali mbaya ya uchafu. Kama ushuru unakusanywa kila siku, pesa zinaenda wapi? Mbona hatuoni matokeo yoyote?

Kibaya zaidi, Wafanyabiashara wanasema walipewa eneo tu, lakini mabanda walijenga wenyewe kwa gharama zao, hii imeibua maswali miongoni mwao, wakidai wanatozwa ushuru kwa mabanda waliyoyajenga wao wenyewe.

“Hivi, ushuru ni wa mabati, mbao, au mazingira machafu? Serikali ituambie ili tujue” hizo ni baadhi ya kauli za Wanafanyabiashara wa hapo.
IMG_20250108_145812_766.jpg
Magonjwa ya Mlipuko na Hali Mbaya ya Afya
Soko hili limekuwa chanzo cha magonjwa ya mlipuko. Mwaka 2023, inadaiwa watu wawili walifariki kutokana na ugonjwa wa Kipindupindu, huku wengine wakikumbwa na magonjwa ya kuhara.

Uchafuzi wa mazingira na ukosefu wa miundombinu ya usafi umechangia kwa kiasi kikubwa hali hii mbaya.

Wafanyabiashara wanasema kuwa magonjwa haya yamekuwa sehemu ya maisha yao. "Tunaugua mara kwa mara, lakini hatuwezi kusimamisha biashara zetu. Tuna watoto wa kulea, na Serikali haionyeshi nia ya kutatua tatizo hili," alisema mmoja wa wafanyabiashara.
IMG_20250108_145812_596.jpg
Serikali Imepoteza Dira?
Wafanyabiashara wamekuwa wakitoa kilio chao mara kwa mara kwa viongozi wa soko, halmashauri ya wilaya, hata wenyeviti wa mkoa. Pamoja na yote, majibu wanayopata ni yale-yale: "Tutalishughulikia." Muda unazidi kusonga, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa.

Badala ya kuwasaidia, baadhi ya viongozi huwatishia wafanyabiashara wanaolalamika. "Ukiongea sana, wanakuambia utafute soko jingine. Lakini huu ni mtego, kwa sababu hakuna mahali pengine pa kwenda," alisema mfanyabiashara mmoja kwa masikitiko.

Uoga Unatamalaki
Licha ya hali mbaya sokoni, wafanyabiashara wengi wameamua kukubali hali hiyo kutokana na hofu ya kufungiwa meza zao. "Tulijaribu kugoma mara moja, lakini tulionywa kuwa meza zetu zingebomolewa. Tumeamua kunyamaza tu na kuendelea na biashara," alisema mmoja wao.

Hali hii ya kukosa matumaini imewafanya wafanyabiashara wengi kuendelea kufanya biashara katika mazingira haya machafu. Uchafu unazidi kuongezeka, na harufu mbaya imekuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku.

Suluhisho Lazima Lipatikane
Hali ya Soko la Kayenze inahitaji hatua za haraka, Wafanyabiashara hawa siyo tu wanastahili mazingira safi na salama, lakini pia wanapaswa kuona thamani ya ushuru wanaolipa.
IMG_20250108_145812_385.jpg
Serikali ya Wilaya ya Magu inapaswa kuwajibika kwa kuhakikisha dampo linahama, mtaro wa maji machafu unatengenezwa, na mazingira ya soko yanaboreshwa kwa ustawi wa wajasiriamali na wateja.

Soko hili ni mfano halisi wa kushindwa kwa mifumo ya usimamizi wa biashara ndogo ndogo nchini.

Je, tunasubiri mlipuko mkubwa wa magonjwa ili hatua zichukuliwe? Serikali inapaswa kusikili
za kilio cha wafanyabiashara wa Kayenze sasa.
 
Hii ni aibu na hatari kwa usalama na afya za wananchi. Unless hatujitambui, wanaouhusika wawajibike na kuweka mazingiza sawasawa.

Daah..nikiona vile vitambi vya wakubwa na kuna mambo kama haya yanaendelea najiuliza, uongozi ni kwenye timu tu ya Pamba wakati inacheza na Simba?
 
Hii ni aibu na hatari kwa usalama na afya za wananchi. Unless hatujitambui, wanaouhusika wawajibike na kuweka mazingiza sawasawa.

Daah..nikiona vile vitambi vya wakubwa na kuna mambo kama haya yanaendelea najiuliza, uongozi ni kwenye timu tu ya Pamba wakati inacheza na Simba?
Amini kwamba Mzee wangu
 
Back
Top Bottom