unalima breed gani ya boga, maboga yapo ya aina nyingi mkuu. mbegu za maboga ni dili kwa nchi za uarabuni.
changamoto ni wakulima hawana uwezo wa kukidhi vigezo vya mnunuzi. ili uweze kuexport kuna vigezo mnunuzi anatoa kuanzia aina ya boga, moisture, ujazo na uweze kusuply kwa muda ambao wao watahitaji
Kuna mzee ana kampuni na alipata tenda ya kusuply huko uarabuni, ishu ikawa anashindwa kupata tani wanazozihitaji kwa muda waliopanga. mfn supplier uwe na uwezo wa kusuply container 4 za futi 40 kwa mwaka mara nne. Huo mzigo unapata wapi? Alijaribu kuwahusisha wakulima wengine ili anunue mzigo kutoka kwao, lakini njaa inawafanya wanauza nje ya makubaliano. Tenda ilimshinda mkataba ukavunjika
mazao mengi yanahitajika nje, changamoto ni kukidhi standards zinazohitajika na wanunuzi.
Kwenye maboga tukiwa na kilimo cha pamoja, kuhusisha watu wengi ili ulkukidhi demand ya mnunuzi inawezekana. Ukisema ni kuingia kivyakovyako ni ngumu aisee.