Iamabdulkareem
Member
- Jan 25, 2018
- 16
- 48
Acha niandike lile ambalo nimeliona kwa hizi siku za karibuni, si mzuri sana katika uandishi hivo kwenye makosa mtanisamehe.
Awali ya yote heshima yenu wakuu natumai siku imeanza vizuri kwa wengi na wale wenye matatizo Mungu awabariki wapate unafuu kwenye matatizo yao.
Acha niende kwenye point nikiongelea industry yetu ya mziki Tanzania kama mdau ninaefuatilia kwa ukaribu.
Miaka ya karibuni baada ya kudrop kidogo miziki ya aina ya Dance pamoja na Taarabu ikapelekea kuingia kwa kasi zaid mziki wa bongo flevour katika soko na kupendwa na wengi zaid hasa vijana pamoja na rika lingine. Kwa nchi yetu Tanzania wasanii mbalimbali mfano Diamond na team yake wamejitahidi ktk kuupeleka zaid kimataifa hongera kwao.
Changamoto kubwa niliyoiona kwa miaka miwili ya hivi karibuni bongo flevour imekuwa ya ushindani zaidi ambapo naona kabsa inapoelekea either industry inaweza kwenda kufa au baadhi ya wasanii kupotea kabsa na kuacha wachache pekee. Wasanii wanajitoa sana katika kutoa mziki kwa sasa kila mtu anajaribu kuonesha kile ambacho anafanya ili watu na wanadau waweze kuwaona ila matokeo yake yamekuwa tofauti kidogo kwa sababu ndani ya siku moja utakuta wasanii takriban hata kumi wanatoa nyimbo, hii ni kwa wote wasanii wachanga na wanaochipukia na wakubwa wote unakuta wanatoa nyimbo kwa siku moja.
Kwangu mimi naona inapelekea watu kushindwa kuwapa nafasi wasanii wote kuwasikiliza kwa kile walichotoa, ushindani huu kwa maoni yangu naona yanapelekea watu kutazama zaidi kazi za wasanii wakubwa tu na kuzi ignore kazi za wasanii wachanga hii pia inaweza pelekea kuua industry ya mziki wa bongo flevour kwa miaka ya baadae.
Maoni yangu hasa kwa wasanii wakubwa kutoa mziki back to back ni nzuri ila kwa vile wao wanakuwa wanafuatiliwa zaid na washajizolea mashabiki wakutosha naona wangekuwa wanaweka interval kidgo ya mda ili kuwawezesha na wasanii wengine kutoa kazi zao na kusikika kwa wananchi.
Je ww pia kama mdau wa mziki una maoni gani katika suala hili. Karibu kukosoa na kutoa maoni