Soko la mziki limekuwa la ushindani, wapi linapoelekea

Joined
Jan 25, 2018
Posts
16
Reaction score
48
Acha niandike lile ambalo nimeliona kwa hizi siku za karibuni, si mzuri sana katika uandishi hivo kwenye makosa mtanisamehe.
Awali ya yote heshima yenu wakuu natumai siku imeanza vizuri kwa wengi na wale wenye matatizo Mungu awabariki wapate unafuu kwenye matatizo yao.
Acha niende kwenye point nikiongelea industry yetu ya mziki Tanzania kama mdau ninaefuatilia kwa ukaribu.

Miaka ya karibuni baada ya kudrop kidogo miziki ya aina ya Dance pamoja na Taarabu ikapelekea kuingia kwa kasi zaid mziki wa bongo flevour katika soko na kupendwa na wengi zaid hasa vijana pamoja na rika lingine. Kwa nchi yetu Tanzania wasanii mbalimbali mfano Diamond na team yake wamejitahidi ktk kuupeleka zaid kimataifa hongera kwao.

Changamoto kubwa niliyoiona kwa miaka miwili ya hivi karibuni bongo flevour imekuwa ya ushindani zaidi ambapo naona kabsa inapoelekea either industry inaweza kwenda kufa au baadhi ya wasanii kupotea kabsa na kuacha wachache pekee. Wasanii wanajitoa sana katika kutoa mziki kwa sasa kila mtu anajaribu kuonesha kile ambacho anafanya ili watu na wanadau waweze kuwaona ila matokeo yake yamekuwa tofauti kidogo kwa sababu ndani ya siku moja utakuta wasanii takriban hata kumi wanatoa nyimbo, hii ni kwa wote wasanii wachanga na wanaochipukia na wakubwa wote unakuta wanatoa nyimbo kwa siku moja.

Kwangu mimi naona inapelekea watu kushindwa kuwapa nafasi wasanii wote kuwasikiliza kwa kile walichotoa, ushindani huu kwa maoni yangu naona yanapelekea watu kutazama zaidi kazi za wasanii wakubwa tu na kuzi ignore kazi za wasanii wachanga hii pia inaweza pelekea kuua industry ya mziki wa bongo flevour kwa miaka ya baadae.

Maoni yangu hasa kwa wasanii wakubwa kutoa mziki back to back ni nzuri ila kwa vile wao wanakuwa wanafuatiliwa zaid na washajizolea mashabiki wakutosha naona wangekuwa wanaweka interval kidgo ya mda ili kuwawezesha na wasanii wengine kutoa kazi zao na kusikika kwa wananchi.

Je ww pia kama mdau wa mziki una maoni gani katika suala hili. Karibu kukosoa na kutoa maoni
 
MKUU KILA JAMBO LINAPASWA KUWA NA USHINDANI ILI KULETA MAENDELEO KATIKA FANI HUSIKA.TATIZO HUKU KWETU USHINDANI UPO KATIKA KUHARIBIANA NA SIO KUJENGANA
 
Ukitoa ngoma kali hata Kama ni underground ngoma yako ita hit tu mfano foby na Mario ngoma zao zinafanya vizuri kuliko hata baadhi ya wasanii wakubwa japo wanamda machache kwenye industry ya bongo.
 
hata shuleni kulikuwa na wanafunzi kila swali likiulizwa kinasimama kujibu,mwalimu inabidi amruke na kumchagua mtoto mwingine.ili kuweka ushindani.

sasa nyinyi mmekomaa na wasanii wenu tu hata wawaimbie upupu mmo.kuna nyimbo nzuri zinaimbwa ila wasikilizaji ndio mnafeli.
 
Yah hili linaharibu pia mziki wa bongo fleva kwasababu wengi wetu tumekuwa watu wa kuwasikiliza baadhi ya wanamuziki. Mashabiki tumekuwa wa kuwasikiliza baadhi ya wasanii tu
 
Diamond ndo zake hizo..

Wenzake wakitoa ngoma akiona Kali anaipoteza fasta tuu kwa kuachia dude lake naye..
 
Ushindani ndio unakuza mziki ata Marekani mziki una ushindani mkubwa ndio maana wana tengeneza pesa
 
Ushindani ndio unakuza mziki ata Marekani mziki una ushindani mkubwa ndio maana wana tengeneza pesa
Yah ushindani ni muhimu ktk sekta ya mziki ili sanaa ikie ila sisi mashabiki naona tuna tatizo kubwa la kubagua wasanii wakuwasikiliza.. je hili unalizungumziaje ktk kukua kwa mziki
 
Tatizo lipo kwa mashabiki, wengi wamejilengesha kusikiliza mziki kutoka kwa wale wasanii wanao wakubali. Ikitokea hata underground katoa ngoma kali kuliko ya star ambaye anajina kubwa nyimbo yake itafichwa itakosa wasikilizaji kwasababu wote watakua bize kusikiliza ngoma ya star hata kama mbovu. Na ndio maana nimeona karibia wasanii wengi hapa bongo ndoto yao ni kufanya collabo na wasafi ilimradi ajitangaze kwasababu anajua lebel inajina kubwa hivyo ni rahisi kutambulika


Watu hatusikilizi mziki mzuri watu tunasikiliza mziki kutoka kwa artist tunayemkubali pekee, jambo ambalo linawanyima mwanya wa kutoka hawa underground
 
Kwahili nakubaliana na wewe mkuu kwa asilimia zote. Ukipitia youtube huko unaweza kita nyimbo ni kali sana kutoka kwa underground au wasanii wa kawaida tu yenye views chache.

mimi naona Mbali na underground kujitahid kuomba collabo kwa wasanii wakubwa vlevle naona media zijitahidi kupiga jicho kwa hawa wasanii wachanga bila upendeleo wowote ule ili kiwaboost hawa vijana wanaochipukia sabab c miaka yote tutakuwa na kina ally kiba, diamond na wengineo. Vlevle inabd wapewe nafac pia 7bb media ina nafasi kubwa sana ya kuifanya jamii kuwakubali aina flan ya wasanii.
 
Diamond ndo zake hizo..

Wenzake wakitoa ngoma akiona Kali anaipoteza fasta tuu kwa kuachia dude lake naye..
Sasa na wao wakiona Diamond kaachia ngoma ina bidi waipoteze kwa kuachia ngima kali zaidi...
 
Na hii ndio itaenda kumcost Harmonize,mashabiki wa wcb wamemtenga,sasa hivi amekua kituko kujipitisha pitisha mitaani ili aendelee kumantain status...."mziki wa bongo fleva umezidiwa nguvu na team wasafi"
 
Bosi hamna aina ya muziki ambao huwa unakuwa kwenye chati milele hata mfanye nini lazima ushuke uje aina nyingine ukae juu nao ushuke yani watu huwa wanachoshwa tu na aina Fulani wanataka aina nyingine hata ulete ubunifu gani!!...ni swala la muda tu bongo flavor itashuka utakuja muziki mwingine!
 
Ningeshauri kuwepo na kampuni moja (wenye mtaji),wasanii wote wanaotoa nyimbo wazipeleke kwenye hii kampuni.....hii kampuni ndio wawasiliane/wawasilishe kwenye vyombo vya radio,tv n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…