Soko la ndege kware (Quail) lipo

Soko la ndege kware (Quail) lipo

dostum

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
215
Reaction score
110
Salam ndugu wana jamvi.

Nimeona mara nyingi articles zikielezea manufaa ya ndege jamii ya kware. watu wengi wamejaribu kutoa faida zake kem kem zinazohamasisha kufuga ndege huyu.

Lakini ukichunguza taarifa hizo taarifa muhimu muhimu muhimu sana huambiwi nayo kama utaamua kufuga soko la ndege hawa liko wapi? kwa maana ingine wapi liliko soko la uhakika wanakohitajika ndege hawa.

Wenye taarifa wanijuze kwani nakaribia kuwaacha huru baada ya kukosa/kutojua nitaenda kuwauza wapi.
 
dostum

Na hili ni tatizo sana hasa kwa jinsi wachangiaji wanavochangia! huwa mara nyingi ktk mambo mbalimbali huwa zinakosekana taarifa muhimu! hata mimi nilijitahidi kulifuatilia hili suala hapahapa lakini sijapata kujua!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu pole kwa sasa tunafuga kwa ajili ya mayai kwa sababu mayai ndio yamekuwa dili ila kama wewe ulifuga kwajili ya nyama soko hilo bado ni mtihani ila ni muhimu watu waendelee kupata elimu naamini siku moja na la nyama litakuwa juu
 
Ufugaji kwa Kwale (Quail) uko wa aina mbili
1. Kuna hawa Japanese Quails ambao ndiyo wanafugwa sana ukanda huu wa afrika mashariki, na hawa ni maarufu sana kwa mayai kwa kuwa wanataga mayai mengi takribani mayai 300 kwa mwaka lakini umbo lao ni dogo about 250g.
2. Kuna Jumbo Quails ambao hawa ni mahsusi kwa ajili ya nyama lakini utagaji wao wa mayai ni hafifu kidogo hawa hufika hadi 800g.

Kazi ni kwako kama utafuga wa nyama au mayai.

BTW: Kama unahitaji mayai ya Kwale wasiliana nami trey moja ya mayai 30 ni shilingi 20,000/=
 
Back
Top Bottom