Soko la Ndugai lililojengwa Dodoma kwa mabilioni na kuzinduliwa kwa mbwembwe limetelekezwa na wafanyabiashara

Wabongo wanaamini sehemu ikijengwa vzuri basi vitu vitakuwa bei ..ndio maana wana penda sehemu za ajabu ajabu
Tatizo ni kuwapa vizimba/vyumba vya biashara maofisa, wa ofisini wasio na uzoefu wa biashara, wanakaa navyo hawafanyii biashara. Pia Kodi kubwa na mifumo ya kibabe ya kibiashra. Pale (77) sabasaba,, ni eneo zuri sana. Ila soko ni chafu na vibanda kama vya njiwa. Lingevunjwa lote likapangwa ghorofa, mitaro ya maji machafu, pavement, umeme wa uhakika, maji ya uhakika, sehemu za mboga, mitumba, electronics, nafaka, mabenki, butchers, kumbi za mikutano, nk, Dodoma ingeingiza mamilioni kwa siku. Maana ni katikati ya mji. Lakini sasa !!!!!!
 
Legasi za kufosi
 
Cha ajabu waliojenga ni wabobezi wa Engineering, Bussness na Accountancy..
Elimu za bongo nje ya ajira na kupata mshahara sionagi ni wapi zinatumika kufanya mabadiliko.
 
Vp ule uwanja wa ndege wa chato ? Mbuga ? ! Kama nchi tumepitia mengi sana
Nilipita huko kama mwezi 1 hivi sio siri Chato inaenda kuchakaa kwa kasi ya ajabu wale waliojenga kule hawana hamu na hali ilvyo kwa sasa ni vile tu nyumba hazihamishwi.

Viwanja enzi za mzee vilipanda bei lakini kwa sasa vimeshuka bei hadi laki unapata kiwanja huko.

Stand tuliingia ni kama buses zinalazimishwa kuingia ili wapate ile hela ya ushuru ila hakuna bus ndani ya stand hata 1

Taa za barabarani zimeanza kuzima hakuna matengenezo kwa ujumla Katoro pazuri kuliko wilayani Chato.

Nyegezi na Nyamhongolo vyumba vipo wazi tu.
 
Hii ingetufundisha kupanga miji kivipaombele na kimkakati. Leo watu watakimbilia kununua Pemba (japo najua ni vigumu) kwa kuwa miradi mikubwa inapelekwa huko, keshokutwa unaibuka mji mwingine kutokana influence ya Kiongozi, watu wanahama. Sina hakika utalikuta hili Marekani, ulaya au Asia au popote zaidi ya Tanzania. Tungepanga miji ya vyuo, miji ya viwanda, maeneo ya utalii maeneo ya utafiti,.kibiashara nk. Sasa kila nyumba inayojengwa, kuna frame ya duka utafikiri ni sheria ya ujenzi. Jambo lingine ni kupima ardhi yote kwa makazi. Mashamba yanakufa au malisho ya mifugo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…