Soko la Sido laungua moto jijini Mbeya

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Soko la sido jijini Mbeya linaungua moto muda huu.

Taarifa zaidi zitakujia kadri zinavyopatikana.

Your browser is not able to display this video.

Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka kwa Ripota wetu jijini Mbeya,zinaeleza kuwa Soko la Sido lililopo mkabala na maeneo ya Mwanjelwa linateketea kwa moto hivi sasa,Taarifa zinaeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa.

Kwa mujibu wa Ripota wetu aliyepo eneo la tukio,anaeleza kuwa Moto huo ulianza kuwaka mnamo majira ya saa tatu usiku huu na kusababisha tafrani kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwepo maeneo hayo,ambao nao walionesha juhudi zao za kushriki kuuzima,lakini kwa bahati nzuri kikozi cha zima moto kikawa kimeishawasili na kuendelea kupambana na moto huo uliokuwa ukiwaka kwa kasi kubwa mpaka hivi sasa tunapoingia mitamboni.

Kama vile haitoshi katika kuongeza nguvu za kiusalama eneo hilo,Kikosi kutoka jeshi la Polisi la mjini Mbeya tayari nalo liliwasili katika eneo hilo katika suala zima la kuhakikisha ulinzi na usalama wa mali za watu unaimarika .

----
TAARIFA YA AWALI KUUNGUA SOKO LA SIDO JIJINI MBEYA

Natoa pole kwa wote walioathirika na janga la moto kwa wafanyabiashara soko la Sido. SOKO la sido lilianza kuungua saa 21.32 Hrs jana usiku na kuteketeza mali za wafanyabiashara wa soko la sido.

Pamoja na kutoa pole niwashukuru wananchi, vyombo vya ulinzi kwa ushirikiano na kazi kubwa YA kudhibiti moto usiendelee kuleta madhara makubwa zaidi.

Serikali kupitia Mkuu wa wilaya YA Mbeya imeunda kamati YA kufanya tathmini YA kujua hasara na chanzo cha Moto huo.

Tunaomba wananchi waendelee kuwa watulivu na watoe ushirikiano kwa kamati hiyo ili tuweze kujua chanzo cha moto na hasara iliyopatikana.

Aidha vyombo vya ulinzi vinaendelea kuchunguza kujua kama moto huo utakuwa umesababishwa na mtu/ watu uchunguzi huo bado unaendelea.

Nirudie tena kuwapa pole wote walioathirika na janga na mungu awatie nguvu ktk kipindi hiki Kigumu.

Amos G.Makalla
Mkuu wa mkoa wa Mbeya

Pia soma: Soko la Kariakoo lateketea kwa moto
 
Conspiracy, says you must be where you should be
 
Taarifa ya usiku huu kuwa Soko la Sido Mjini Mbeya linawaka moto usiku...Taarifa wamepenyezewa Clouds Redio muda huu.

Sorry ktk mada ni soko siyo solo
 
Tupe taarifa na picha mkuu....sasa tutaonaje mishemishe hapo Dox...
 
duh... na zile frame zao za mbao si kesho patakuwa ni majivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…