Tanganyika1
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 423
- 90
Soko zuri la kueleweka la vitunguu liko kenya, hasa mombasa utapiga hela ya kueleweka.
ukisha uza vitunguu vyako unaweza rudi na karoti manake kenya karoti ni nyingi sana ukaja kuuza hapa bongo.
Hii biashara inalipa sana, nakumbuka mshkaji wangu alikuwa anapiga hzo busnes saiv anamiliki kampun ya tours arusha na bado ana mashamba ya vitunguu huko babat mang'ula
mmh kwa hiyo issue ya kenya/mombasa nadhani msimu ujao kama nitaongeza shamba. mana kwa sasa sidhani kama ntapata zaidi ya gunia 50. ila asante kwa kunifunua macho ntajaribu kufuatilia hilo soko.
Poa mkuu, ila hata hizo gunia 50 si haba! Pia unaweza kuchanganya na mwenzako ili kurahisisha logistics kwa kuwa na mzigo mkubwa na kuchukua gar moja.
tatzo bongo ujuaji sana! Utazungushwa na madalali kibao ambao wanataka cha juu ale pgqawa na wewe ulievuja jasho kulima had kusafirisha mazao had sokoni. Huo ubabaishaji na usumbufu wa madalali bongo ni kero sana na wanaleta unyonyaji ndo mana nkakupa option ya soko la jiran hapo ambalo lina uwazi na hakuna longo longo. Pia currency yao iko stable kidogo.
Hilo nalo neno. unajua hapa kwetu sijui ni lini watu tutabadirika. mana kila ukijitahidi kujisogeza utaona mtu kwa waziwazi anataka kukurudisha nyuma. ngoja kuna mdau mmoja hapa nae kalima ngoja nimcheki nione tutafikia wapi. Asante sana mkuu
Hivi Mangula iko babati?Mangula kwa vitunguu inalipa sana but duh masharti ya ulimaji huko nako ni magumu.Soko zuri la kueleweka la vitunguu liko kenya, hasa mombasa utapiga hela ya kueleweka.
ukisha uza vitunguu vyako unaweza rudi na karoti manake kenya karoti ni nyingi sana ukaja kuuza hapa bongo.
Hii biashara inalipa sana, nakumbuka mshkaji wangu alikuwa anapiga hzo busnes saiv anamiliki kampun ya tours arusha na bado ana mashamba ya vitunguu huko babat mang'ula
Hivi Mangula iko babati?Mangula kwa vitunguu inalipa sana but duh masharti ya ulimaji huko nako ni magumu.
ndugu yangu,, mimi nimuathirika wa soko la vitunguu,, nilirudi home nikaingia kichwa kichwa kwenye biashara hii nilikwenda ruvu darajani,, nikaenda mpwapwa,, kote huko nimembulia hasa tena hasara kubwa sana,, nilianza na mtaji wa gunia 90 mwisho kabisa nikawa na uwezo wa guni 18 mtaji ukakata,, soko la kariakoo usiguse utajuta pale kuna watu wasio binadamu kabisa na wanaijua biashara hii,, watakuliza utalia nimelia kidogo niumbuke mjini,, wakati watu bado wanajua ninahela tayari vitunguu vilikuwa vimeshanikata,, na sio tatizo la soko la,, ni wizi ndo issue unaibiwa unaona,, hupangi bei mwizi ndo anaekupangia bei,,sina ya kusema ila kama umelima mwenyewe uzia shamba baaas
Mkuu pole sana,
Ni kweli biashara ya kitunguu inalipa sana, tatizo liko ktk mfumo wa uuzaji, hasa kwa mkulima anayeleta toka shambani na kuwakabidhi wale manyangumi pale k/koo. Hawa wezi hawako ktk kitunguu tu, biashara karibu zote zimeingiliwa na hawa watu wa kati. Wakulima lazima tujipange namna ya kuondoa hawa wezi kwa kuwa na ushirika wa wakulima ktk vikundi kwa location tofauti tofauti.
Mfano, Ruaha Mbuyuni wakulima wa kitunguu wakiwa na ushirika wao,wakawa na pembejeo zao na bei zenye tija itasaidia sana, kadharika na huko Mang`ola Manyara au Kibakwe, mwisho itakuwa ngumu kwa manyang`au kumfikia mkulima na kumliza.
Kijijini kwetu kuna kijana amehama kijiji kwa sababu ya viazi, alileta kiazi k/koo, yaliyotokea ni historia.
mmh kwa hiyo issue ya kenya/mombasa nadhani msimu ujao kama nitaongeza shamba. mana kwa sasa sidhani kama ntapata zaidi ya gunia 50. ila asante kwa kunifunua macho ntajaribu kufuatilia hilo soko.