Soko la vitunguu Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania

Soko la vitunguu Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania

Smarter

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2008
Posts
528
Reaction score
114
Salaam,
Natafuta soko la vitunguu popote East Africa, Niko tayari kuuza gunia kwa Tsh 95,000/= kama order ni kubwa sana mpaka Tsh 120,000/=. ( Bei inaweza kuongezeka yote yanategemea na uko wapi na utapenda kununulia nilipo au kuletewa). Nafanyia Production Mkoa wa Arusha na Kilimanjaro.

Nakaribisha Mawazo,
 
Peleka vitunguu somalia ila ujipange vizuri nunu AK 47 kwanza usikubali kuuza kwa hela yao tumia USD
 
Mkuu ungeipeleka kule jukwaa la business mule wamejaa wajasiria mali
 
Tandale au Tandika kama upo pande za Dar, km upo Sumbawanga peleka Sokomatola, kama upo Mbeya peleka Mwanjelwa,kama upo Kilimanjaro peleka Memorio kama upo mkoa mpya wa Katavi peleka Kashaulili, kama upo Arusha peleka kwa Mlomboo maana wanachoma nyama huenda wakavihitaji kwa ajili ya kutengenezea kachumbari na kama upo mkoa mpya wa Simiwi peleka Lamadi
 
ni vizuri ukalipeka tangazo lako mahala husika.Amani kwako
 
kama unaweza kaangalie soko zanzibar, nilimkuta dada mmoja anavitoa babati analeta kule kuuza kwa kwa magunia ila sikumbuki bei yake ilikuwa kiasi gani. Kule vitunguu hamna vina soko nnavyosikia
 
Smarter - hii inaniuma maana kama mzalishaji ilibidi uwe na access nzuri kwa msoko. Kitunguu chekundu grade A kina soko sana nje ya nchi. US wanauza hadi $4 kwa kilo 1.5 (i.e. 3 pounds) wakati cheupe hakipati hiyo bei. Nafikiri ni muda muafaka kwetu waTz kuwania masoko ya ulaya na hivyo kuongeza nguvu ili tutoe mazao yenye kiwango cha juu.
 
mandieta
wew ni mkulima??kam ndio naomba uni PM tubadilishane mawazooooo
 
Helow wana jamii forums,

Naombeni mnisaidie maoni au kuni unganisha na watu watakao itaji vitunguu vya jumla. Vitunguu vinatoka moja kwa moja kutokea mkoani. Magunia yapo mengi zaidi ya 100. Kwa mawasiliano zaidi. 0778- 480905 (what's up) 0716-369299 (txt / call)

Sent from my BlackBerry 8520
 
Helow wana jamii forums,

Naombeni mnisaidie maoni au kuni unganisha na watu watakao itaji vitunguu vya jumla. Vitunguu vinatoka moja kwa moja kutokea mkoani. Magunia yapo mengi zaidi ya 100. Kwa mawasiliano zaidi. 0778- 480905 (what's up) 0716-369299 (txt / call)

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
aina gani ya vitunguu? .... kama ni 'Red Bombay' soko lipo kenya ukipeleka tarakea rombo wananunua wafanyabiashara wa kenya
 
Back
Top Bottom