amini usiamini, nilipokuwa nafanya kazi kama state attorney, kabla sijajitoa na kuwa mwanasheria wa kujitegemea, mwaka mzima nilikuwa situmii/sigusi kabisa mshahara wangu. mshahara hauguswi, napata pesa tu zinakuja ndo za kutumia. nikienda mahakamani asubuhi, lazima nirudi na pesa...si lazima rushwa, wakati mwingine mtu tu umeamua kumwachia labda kwasababu umeona hakuna ushahidi kwenye kesi yake, kesho yake unashangaa anakuletea laki mbili za shukrani, anakushukuru wala hujaomba....cha muhimu ni kukaa vizuri na watu. achilia mbali hizo traffick case, dhamana etc, kuna mianya mingi ya kupata pesa, ambapo hata kama wewe si mla rushwa kama mimi, ukimfanyia mtu fadhila, lazima anaenda kurudi...nilijikuta naishi bila kugusa mshahara wangu....nilisomesha watoto, nilifanya mengi, nje ya mshahara.....chukulia mfano, mwanasheria wa serikali grade ya kwanza au ya pili kwasasa anapata si chini ya laki nane kwa mwezi, lakini hiyo laki nane nakwambia haigusi, kuna pesa nyingine nyingi zinazunguka ofisini kila mwezi, akisafiri kidogo tu analipwa perdiem,
akipanda kidogo tu akapata kuwa senior state attorney, analipwa milioni, akifika principle state attorney analipwa milioni na nusu au zaidi...sasa hizo ni mishahara ya serikali,cha ajabu ni kwamba, unapata hela nyingi zaidi nje ya mshahara, ukijaunganisha, unashangaa karibia mara tatu ya mshahara wako kwa kwezi......ukishapata experience, ndo unajiondoa kama sisi, unaunda lawfirm yako ya kawaida, mtu kumsimamia tu kesi zilizo nyingi anatakiwa aje na milioni na nusu au zaidi....hapo kumsaidia, milioni mbili, tatu, nne hadi ishirini kutegemeana na kesi...cha ajabu, kwasababu mimi nimefanya kazi hiyo mda mrefu, kile kitu ambacho mimi naona rahisi kupita vyote, mwenzangu ananipa pesa ili nikamsimamie, hivyo pale naenda kama marejeo tu ili kukamilisha nipate ile pesa kwasababu karibia kesi nyingi ninazosimamia, kipindi cha nyumba niliwasahi kutana nazo na kusolve tatizo hilo zaidi ya mara hamsini...
kuwa layman/kutojua sheria ni mzigo mzito usiobebeka...nawahona huruma...yaani kile wewe unachoogopa sana kwenda hata mahakamani, kuongea mahakamani, kujitetea au vile usivyojua sheria,,,,mimi mwenzio naona ni kutu rahisi kupindukia....kwenda mahakamani ni sawa tu nawewe unavyoenda kwa kuchez a pool pale kwenye bar ya masawe.....hahaha.