Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kama ilivyowahi kusemwa kuwa mafanikio ya kivita ya Ukraine kati yake na Urusi kuwa namba zake huenda hazipigwi kwa base ten kwani daima huwa ni makubwa mno kuliko uhalisia unaonekana.
Wiki iliyopita Ukraine ilitangaza kupiga makao makuu ya jeshi la majini la Urusi kwenye bandari ya Sevastopot yaliyopo bahari nyeusi.Kituo hicho ni muhimu sana kwa Urusi na ni moja ya lengo kuu la Ukraine kuidhoofisha Urusi.
Katika tangazo lake hilo Ukraine ilisema ilifanikiwa kusambaratisha makao makuu ya jeshi hilo na kuu makamanda 34 miongoni mwao akiwa ni mkuu wa jeshi hilo la Urusi Admiral Viktor Sokolov.
Baada ya kutangazwa mafanikio hayo ya Ukraine ambayo yalikuwa yakirudiwa kila saa, Urusi kwa upande wake haikujibu chochote, Siku tano mbele yake Viktor akaonekana kwenye video akishiriki katika mkutano na waziri wa ulinzi wa Urusi.
Picha hiyo iliwatia kizaazaa kikubwa viongozi wa kijeshi wa Ukraine waliotoa matangazo hayo waliyosema wameyathibitisha kuhusu vifo hivyo.Hilo liliwafanya waanze kujifariji na kujitoa kimaso maso kwa kusema aliyeonekana kwenye video hiyo ni yeye kamanda Sokolov lakini huenda ni picha ya zamani na kama ni ya karibuni basi ilikuwa ya maiti yake au akiwa kitandani hospitali.Dalili walizotoa za kuaminisha hilo ni kwa vile kwanza admiral Sokolov katika video hiyo hakuwa akisema, macho hayafumbi na kufumbua na nyuma yake alikuwa amewekewa mito.
Muda huo waziri wa ulinzi wa Ukraine alihojiwa kwamba mbona kuna tetesi kuwa kiongozi wa jeshi la maji la Urusi yuko hai na jee ana kipi cha kusema.Akajibu kwamba ikiwa amekufa itakuwa ni bora zaidi.
Siku ya pili yake admiral Sokolov akatokea mwenyewe wote mzima kwenye mkutano na waandishi wa habari na alipotakiwa aeleze chochote kuhusiana na shambulio la Urusi kwenye ofisi zake za Sevastopol, akuliza kwani kulitokea nini.Hakumbuki kilichotokea.
Baadhi ya vyombo vya habari vimempatia jina la kamanda wa vita aliyefufuka.