Sokwe wa kufoji vs simba dume.

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,656
wana JF hii sijui kama mliipata ila sio mbaya nikawaletea hasa kwa baadhi ambao hamjaipata. Ni Hivi.....

Kuna Jamaa mmoja alienda kuomba kazi katika zoo moja.
Kazi alipata lakini Meneja wa ile zoo alimpa sharti moja kuwa, Pale kwenye zoo kulikuwa na Sokwe ambaye alikuwa ni kivutio kikubwa sana kwa watalii hasa wa kigeni.
Bahati mbaya yule sokwe alikufa na hivyo kusababisha kupungua kwa wateja na kushuka umaarufu wa ile zoo.
Hivyo kazi ya yule jamaa ilikuwa ni kuvaa maski na ngozi kama ya sokwe na ajifanye yeye ni sokwe ili kurudisha hadhi ya ile zoo.
Kweli kazi ilifanyika, jamaa aliimudu kweli kweli na zoo ikarudisha hadhi yake.
Kijumba cha yule jamaa 'sokwe' kilikuwa juu ya kijumba cha simba dume (kama kighorofa flani hivi).
Siku moja watalii wakiwa wamejaa katika zoo kumwangalia 'sokwe' mpya,
katika makeke ya kisokwe bahati mbaya floo iliyotenganisha kijumba cha sokwe na simba ikaharibika na kusababisha 'sokwe' kuporomoka na kuingia katika kijumba cha simba.
Sasa ana kwa ana, 'Sokwe' na simba.
'Sokwe' akaona mambo yameshaharibika lolote na liwe, mbele ya simba!! Maisha kwanza mengine baadaye.
'Sokwe' akaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada "mamaaa nakufaaa....simbaaa.... niokoeni jamaniiiii......"
Simba akamsogelea karibia na sikio kwa sauti ya chini akamwambia "....dogo acha ujinga, usipige kelele...tutafukuzwa kazi!!...."




TCHAO
 

Du kiboko..
 
Personally niliipata ila thanks anyway
 
Hapo baba kiama lazima upige kele na huyo simba kumbe ni sela wake,duh patamu hapo sana tuuu...
 
take time to laugh, is the music of soul
 
....Oh my God I'm laughing like crazy, uwiiiiiiiiiii hahahahahahh!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…