Hizi sola mimi bado sizielewi vizuri. Pamoja na matatizo yote ya TANESCO, bado sola haijapata kushika soko. Nafikiri ina mushkeli fulani. Aidha katika gharama za matumizi au upatikanaji wa taa na vitu vingine vya sola. Siku moja nilienda kuulizia mambo ya sola karibu na gerezani, nikakuta agent mwenyewe anatumia tanesco, kumuuliza kulikoni hana jibu!!
Hebu wadau mliokwisha tumia sola tuambieni, inafaa?