Soma hapa ili kufahamu kuhusu dhana ya Awamu ya Sita kama inavyotumiwa na Rais Samia

Soma hapa ili kufahamu kuhusu dhana ya Awamu ya Sita kama inavyotumiwa na Rais Samia

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Wanabodi!

Wengi wanaamini Rais Samia Suluhu Hassani hayupo sahihi kusema yeye ni Rai's wa awamu ya sita.

Kutokana na watu wengi kuwa na mkanganyiko juu ya suala hili naomba nifafanue Kama ifuatavyo.

Nafikiri Kwanza tujue maana ya neno lenyewe " Awamu" Kimaana neno hili haliendi kinyume na neno "Zamu" , "Zama" ama kipindi" au "nyakati" .

kila " Awamu" katika Serikali huwa na "mkuu" wake yaani Rais. Kwa muda wote atakaokaa madarakani huunda awamu yake moja (kiutawala).

Kwa mujibu wa katiba Rais mmoja anaweza kuwa "mkuu" wa serikali Kwa "awamu" mbili lakini Kimantiki huwa ni awamu moja iliyogawika katika vipindi yaani A na B, hivi vipindi viwili Kama mechi moja ya mpira wa miguu. ambapo kila "kipindi A na B" kina miaka mitano Kama dakika 45 za soka (na hapa ndipo wengi pamewachanganya).

Awamu ya Kwanza " mkuu" wa serikali alikuwa JK Nyerere aliyeongoza "awamu" moja yenye jumla ya miaka 23. Nyerere alipostaafu " awamu" , "Zama" ama wakati wake ukaishia hapo.

Ikajaja "awamu " ama "Zama" za Alhaji Mwinyi ambayo ilidumu Kwa miaka "10" awamu ya Mwinyi iliisha Kwa yeye kumaliza mda uliowekwa kikatiba.

Ikaja awamu ya tatu na ya nne zilizoisha Kwa namna Kama ya Mwinyi.

Ikaja awamu ya tano iliyoongozwa na JPM ambapo awamu yake imedumu Kwa takribani miaka sita , awamu ya JPM imeisha Kwa yeye kufariki (R.I.P) kabla haijakamilika miaka iliyowekwa kikatiba Kwa awamu moja. Rais akifarik na "Zama" , wakati wake wa kutawala huishia hapo.

Kifo kimekatisha awamu ya utawala wa JPM na kutulazimisha kuingia awamu ya "sita" ya Rais Samia Suluhu Hassan. Awamu za uongoz hazibadiliki Kwa uchaguzi pekee Kama wengi walivyokariri bali zinaweza kubadilika Kwa Rais wa awamu husika kujiuzulu "kung'atuka" , kumaliza kipindi chake kikatiba na Hata Rai's kufariki.

Mama Samia ni rais wa awamu ya sita.

Naomba kuwasilisha.

Orketeemi

 
Wako watu humu wana vichwa vigumu sana kuelewa hili kwa sababu ya mahaba ya mwendazake
 
Kuna jama mmoja ni kilaza wa hali ya juu anakuja humu...
 
Wako watu humu wana vichwa vigumu sana kuelewa hili kwa sababu ya mahaba ya mwendazake
Na cha ajabu eti kuna mwanasheria nguli sijui kilaza gani eti naye anasema rais wa sita lakini awamu ya tano yaani wasomi wa bongo bwana.
 
Umeileza vizuri sana imeeleweka anakataa hoja yako hii huyo ni mbishi tu sasa

Kwa kifupi kila zamu ina Wakati/Kipindi wake/chake. Zamu ya JIWE ilikua ni wakati wa kipindi cha tano cha uongozi wa nafasi ya uraisi

WAKATI = Sehemu ya muda fulani mfano "wakati wa ASUBUHI, MCHANA, JIONI" au "wakati wa TUKIO flani kama Ibada, kuangalia wagonjwa n.k

KIPINDI = Idadi ya sehemu ya muda fulani mfano "kutakua na vipindi viwili asubuhi" au "kutakua na vipindi vitatu vya kuona wagonjwa ambvyo vitakua WAKATI wa ASUBUHI vipindi viwili na JIONI kimoja"

ZAMU = Nafasi ya mtu katika WAKATI au KIPINDI fulani

AWAMU = Utambulisho wa Jina la WAKATI/KIPINDI/ZAMU kwa kizio cha namba kama vile awamu ya kwanza, pili, tatu ...

Hivyo inaweza kusemwa kwamba WAKATI wa uongozi wa MAGUFULI, aliekua akiongoza ZAMU yake kwa AWAMU ya tano, katika kipindi cha miaka kumi, ambayo halumaliza.

Sasa ni ZAMU ya SAMIA kwa AWAMU ya sita ya uongozi katika kipindi cha miaka mitano iliyobaki
 
Back
Top Bottom