Soma Hapa Kama Unataka Kuanzisha Au Kukuza Biashara Yako – Sehemu Ya Kwanza

Soma Hapa Kama Unataka Kuanzisha Au Kukuza Biashara Yako – Sehemu Ya Kwanza

guojr

Member
Joined
Dec 4, 2015
Posts
62
Reaction score
95
Habari ya muda huu wana jukwaa, leo ningependa kuwapa faida ya namna ya kuanzisha au kukuza biasra kwakutumia mbinu ambazo zinafanyakazi hasa katika mazingira yetu ya kiafrika.

Wengi wetu tunapotaka kuanzisha biashara tunajiuliza kuwa ni biashara gani inalipa ili uweke pesa zako zikupatie faida. Fikra ya namna hii sio sahihi na ndio inafanya wafanyabiashara wengi kuwa watumwa wa biashara zao, yaani wanatumia muda na nguvu nyingi kupata pesa kwenye biashara zao. Hata hivyo wengi wanakata tamaa na kuishia njiani bila mafanikio.

Jambo ambalo unapswa kulifahamu ni kuwa biashara ipo katika makundi makuu mawili, kundi la kwanza ni biashara ya kununua bidhaa kwa bei ya jumla na wewe kuja kuuza kwa bei ya rejareja ili upate faida. Biashara ya namna hii ni kama vile kuwa na duka la nguo, nafaka, bucha, dawa na zinazoendana na hivyo. Kundi hili ndio watu wengi tupo humu, na ubaya wa biashara ya namna hii ina ushindani mkubwa sana. Ili upate pesa nzuri lazima ufanyekazi sana ili washindani wako wasikupoteze.

Kundi la pili ni lile linalofanywa katika mtindo wa kitaalam kama vile wataalam wa fitness, chakula, michezo, elimu, utabibu na nyingine zinazoendana na hizo. Biashara ya namna hii inapesa ndefu sana kwasababu wateja hununua bidhaa hata ikiwa bei ghali kwakua wanamwamini kama mtaamu, ndio utasikia mtu aliuziwa asali iliyoweka vitunguu kwa laki 8 sababu aliamini amenunua dawa kwa mtaalam wa tiba.

Je utafanyaje hii biashara ya kitaalam? Fanya mambo yafuatayo ili nawe uwe mtaalam kwenye biashara, ila usinielewe vibaya nikisema mtaalam kwani simaanishi ni lazima uwe umeenda shule na una PhD au una cheti cha professional body kama CPA, la hasha.

Kwanza unatakiwa kujua jamii inachangamoto gani ambazo watu wange toa pesa zao ili kupata utaalam au bidhaa yako. Mfano sasahivi watu wengi wanasumbuliwa na uzito kupita kiasi, namna ya kupata kipato cha ziada, namna ya kupata masoko n.k. Hivyo basi unaweza kuja na mawazo mengi zaidi ya changamoto zinazoikumba jamii halafu wewe ukija na suluhusho basi mtu atatoa pesa yoyote utakayo itaka as long as hiyo suluhisho ndio inatatua changamoto ya mteja iliyokua ikimsumbua kwa muda mrefu.

Leo niishie hapa, itaendelea…

Sehemu Ya Pili
 
Uzi wa maana ila wachangiaji hakuna. Ingekuwa habari inahusu Mobeto na Riki Rosi wakipelekeana moto Dubai sasa uwii sasa hivi uzi ungekuwa unakimbiza replies 1K+

Ukipata muda weka mwendelezo mkuu. Wasomaji makini tupo [emoji1545]
 
Wadada wa kazi wanasumbua sana, kwahiyo biashara ya day care nayo ni nzuri sana sasahivi, pia unaweza fungua website kwaajili ya ku connect wadada wa kazi na wanaohitaji huduma.
 
Wadada wa kazi wanasumbua sana, kwahiyo biashara ya day care nayo ni nzuri sana sasahivi, pia unaweza fungua website kwaajili ya ku connect wadada wa kazi na wanaohitaji huduma.
Ndio mkuu, Umetoa idea nzuri sana kwa upande huu inaweza kuwa msaada kwa watu wengi.
 
Mawazo mazuri sana yenye tija.hongera sana mwanzilishi ,natamani mada ifike mbali ili wengi tusaidike na haya mawazo mazuri.
 
Back
Top Bottom