⚠️Soma Hii Kama Bado unateswa na Mikopo Kausha Damu Na... unatamani Kujinasua na Kujua Mbinu sahahi za kuweza Kutoboa Kupitia Mikopo_

⚠️Soma Hii Kama Bado unateswa na Mikopo Kausha Damu Na... unatamani Kujinasua na Kujua Mbinu sahahi za kuweza Kutoboa Kupitia Mikopo_

Joined
Jul 19, 2021
Posts
15
Reaction score
52
1. Usikope Fedha Kabla Hujajua Kiasi Cha Riba Unayopaswa Kulipa.

Soma Vizuri Ujue Riba ni Kiasi Gani Na Uone Kama Unaweza Kuilipa au Huwezi, Watu wengi likija suala la kukopa huwa wanakuwa na kimuhemuhe kiasi kwamba hawatullii kufikiria kwa kina.

2. Usikope Fedha Ili Ukaanzishe Biashara.

Kopa Fedha Ili Kuendeleza Biashara Uliyoanzisha na ambayo Imeanza Kukuletea Faida.

Na ukikopa nenda kawekeze fedha katika bidhaa zinazoleta fedha nyingi zaidi ya zingine, yaani zile zinazotoka mara kwa mara.

Hii itakusaidia kutengeneza Profit Nzuri kiasi cha kurudisha mkopo na riba yake.

3. Mikopo Sio Mibaya Hasahasa ukiwa una elimu kuhusu mikopo na madeni inayoitwa "Loans And Debts Management Education"

Mikopo ni moja ya income leveraging tool, nikisema leveraging tool namaanisha kitu kinachokuza kipato.

Na inaitwa "Other People's Money" na matajiri wengi wanajua namna ya kutumia hii.

4. Usikope fedha zaidi ya unayohitaji na usikope fedha kwa sababu tu una "access ya kukopa fedha.

Kama imebidi kukopa kopa lakini usikope zaidi ya ile unayoihitaji, kama unahitaji 3 millions kopa hiyo na sio zaidi, ukikopa zaidi hiyo itakayozidi utaitumia vibya.

Na baadae itakuletea shida kubwa sana.
.
5. Usikope Fedha Ili Kuingiza katika Consuming Properties, yaani mali zinazochukua fedha (liability)

Kopa na ukikopa fedha ipeleke kwenye income generaring assets yaani vitu ambavyo kupitia hivyo vitakusaidia kutengeneza kipato.

Usikope fedha ili kununua TV, Simu, Computers, Gari, Hivo vitaongeza matumizi yako ya fedha na baadae mkopo utakuelemea.

Mwisho; Mikopo ni moja ya njia unayoweza itumia kupata mtaji fedha, na mkopo sio lazima uwe na riba.
.
Kama utakopa kwa ndugu, jamaa na marafiki sidhani kama watakuwekea riba,

ILA...
.
ukikopa katika taasisi zoote zinazohusika na huduma za kifedha LAZIMA KUWE NA RIBA.
.
Japo Riba Zinatofautiana kati ya Taasisi moja na nyingine ndio maana sometimes hata riba ya CRDB inatofautiana na NBC, PBZ, NMB nk.
.
Na....
.
kiashiria kimojawapo kwamba una nafasi kubwa ya kufanikiwa kifedha ni uwezo wako wa KUKOPESHEKA.

Ukijiona hauwezi kukopesheka iwe na marafiki, ndugu na jamaa au taasisi za kifedha basi ujue
.
UNA HALI MBAYA SANA!
.
So, Tengeneza Mazingira Watu waone Fedha zao zikiwa kwako ziko mahali salama,
.
ukifika hatua ya kuweza kupata mkopo iwe ni katika taasisi au kwa watu baki basi jua una HALI NZURI.
.
Na By The Way....
.
Kama Unapenda kujifunza Zaidi Jinsi ya kutoboa Kupitia Mikopo basi Gusa Link Kujipatia Ebook Konki ya Elimu ya Fedha na Mikopo Financial Market
.
Hasta la Vista
.
Habakuki Hussen!
+255676147714

Cc:Isaack Nsumba
 
Back
Top Bottom