Mlolwa Edward
Member
- Nov 1, 2016
- 66
- 64
Kumekuwa na wimbi kubwa sana utapeli, wizi na machapisho ya aibu (explicit pornography) kwenye mitandao ya kijamii hususan facebook. Tumeona account za watu aidha zikitumia kurusha maudhui haya kwenye magroup mbalimbali au hata kupitia account zao wenyewe na kuwa-tag wengine.
Mara zote account hizi zinazorusha machapisho haya huwa zimedukuliwa (hacked) hivyo mara zote ukiona machapisho kama haya usidhani muhusika unaemuona kwenye hiyo account anaudhibiti wa account yake
FUATILIA HAPA KWA UMAKINI WA HALI YA JUU NI NAMNA GANI ACCOUNT HIZI ZINAWEZA KUDUKULIWA. Mara nyingi wadukuzi hawa huwa sio hata wazoefu sana kwenye kudukua kitaalamu lakini huwa tu wanacheza na akili za watu kirahisi kupitia shida zao. Mfano mzuri ni kwenye haya machapisho ya michango ya kazi, na sasa hivi trend ni kazi za UNICEF. Unaona chapisho lina screenshot ya mtu kupokea kiasi cha shilingi milioni kadhaa. Inadukuliwa vipi sasa, hapo huwa kuna namba za simu za mtu unaetaka akuunge na hiyo kazi.
Sasa inakuwa kwamba mtu yule atakuomba namba yako ya simu uliyosajilia facebook au email yako, kisha yeye kule atakacho fanya kukwambia kusubiri utatumiwa verification code kwenye namba yako ambayo utamtumia ili athibitishe ni wewe. Yeye kule ataingiaza namba yako halafu atabonyeza "forget password", maana yake ni kwamba anaongea na facebook kwa niaba yako facebook ikijua ni wewe kwamba umesahau password yako.
Facebook utamtumia muhusika sasa halisi verification code ili aweze kuirudisha account yake. Kipindi hicho chote anakuchatisha vizuri ili usiende facebook ukajua nini kimetokea. Sasa baada ya facebook kutuma hiyo kwenye account yako, huyu tapeli atakuuliza kama umepata ujumbe wowote kutoka facebook wa uthibitisho, utaitikia ndio kama mchango uketiki vile, halafu yeye atakuomba umtumie hizo namba, unatumia bila kujua umemkabidhi kichaa rungu, yeye atabadilisha taarifa zako kuwa zake ili akutoe kabisa maana baada ya kuingiza verification code Facebook humpa mtu nafasi ya kuhariri (EDIT) taarifa zake ili iwe rahisi kuendelea kutumia account yake. MPAKA HAPO, KWISHA HABARI YAKO.
Tunanze na kuyaelezea baadhi ya machapisho ambayo sasa kama muhusika wa kawaidia mwenye account yako unayaona, ili uweze kutambua account iliyo chapisha tayari imedukuliwa:
1. Kwanza kabisa account iliyo dukuliwa huanza kwa kuomba msaada wa fedha kwa ndugu na jamaa wa karibu wa mtumiaji kwa njia ya dharula sana isivyo kawaida.
2. Ukiona machapisho ya pornographia, basi ujue hiyo account imedukuliwa
3. Matangazo ya mikopo ya fedha na vitu mbalimbali kama baiskeli, tv, radio, friji na kadhalika AU vitu bei ndogo kupitiliza, ujue hakuna dereva humo. Na mara nyingi wezi hawa hutumia picha za watu bila ridhaa yao na wezi wengi husema wako ZANZIBAR au DODOMA
4. Picha za watu kutumia hivyo sanasana za wanawake kwamba wanatafuta wachumba. Sio wenyewe hao
5. Ukiona maudhui yasiyoendana na azimio la group, mfano unakuta group ni la kuuza na kununua bidhaa lakini kuna mtu karusha video ya mbwa anaonelea, na mara nyingi unakuta hiyo video ina tags nyingi kutoka kwenye groups mbalimbali ambazo sio hata za Tanzania.
6. Machapisho yanayohusiana na kujiunga na illuminati mara freemason mara
Hapo juu ni baadhi ya tu ya namna ambayo unaona account zinakuwa zimedukuliwa.
Lakini pia wadukuzi hawa vilevile hutumia account fake za kutengeneza wao ili kuendeleza wizi mitandaoni. Mfano machapisho ya mikopo, kazi sana sana za supermarket. Majina kama Jokate, Nandy, Kajala, Dewji foundation na kadhalika hutumika sana. Hao wote huwa ni matapeli.
SASA SOMA HAPA KWA UMAKINI SANA. Kuna trend sasa hivi kwenye mitandao ya kijamii kuona baadhi machapisho kama yafuatayo:
"KAMA MIKONO YAKO HAIKO BUSY, MSHUKURU MUNGU",
"WATU WANGU WATAPITA WATU WANGU WASEMA AMEN",
"MIMI SIO NABII LAKINI........",
"MKE WANGU ANATEMBEA NA BODABODA NIFANYAJE",
"BWANA YESU ASIFIWE",
"USINYWE MAJI BAADA YA TENDO, NIULIZE KWANINI",
Aina hizi za machapisho zipo nyingi kupitiliza yani hapo juu ni alisilimia ndogo sana, na najua wengi wenu huwa mnacomment AMEN na ku-LIKE bila kujua kilichopo ndani, mara zote post kama hizi huwa zina PORN attachments. Sasa basi we mama, wewe baba, wewe kaka, wewe dada , unavyocomment hivyo gonga hilo like, au kuitikia AMEN ni kwamba unaiboost post hiyo ya PORNOGRAPHIA facebook kuona kama ina engagement zaidi hivyo kurushwa zaidi na zaidi, na kurushwa kama top ad kwenye groups. Yani wewe unatumika kuwa wakala wa kusambaza pornography bila kujua.
Wito wangu kwa watu ni kwamba waache kukurupuka kuwasiliana na watu wasiowajua maana mitandao ya kijamii inamengi, wengi watatumia uelewa mdogo wa tatumiaji kuwalaghai na kutuma taarifa binafsi. Kama unahisi hauna uelewa zaidi wa mitandao ya kijamii ni mara kumi auche kutumia mitandao hiyo maana taarifa binafsi kuvuja kunahatarisha usalama wako lakini pia wa watu wako wa karibu, jamii husika na taifa kiujumla. Acha tamaa za kutaka vitu kirahisi, mikopo sijui ya riba ndogo, vitu bei ndogo, ajira zenye mishahara mikubwa na kadhalika, utaingia mtegoni na kuingia kwenye matatizo zaidi maana mtu akiwa na udhibiti wa account yako anaweza kushawishi na kufanya lolote kwa sura yako.
LALAMIKO LANGU KWA SERIKALI NA MEDIA. Kwa mtazamo wangu naona serikali imelifumbia sana macho hili tatizo. Post hizi ziko public, kwenye feed kila siku zipo na hata accounts za watu. Kuna mamlaka husika ambayo najua ina watu wa kutosha kufuatilia hili lakini sio watu wakichukuliwa hatua. Mfano post za mikopo, vitu bei ndogo, ajira, mara nyingi unakuta zina na namba za simu. Kwanini namba hizi zisitumike kufuatilia hawa wahusika, lakini pia serikali ku-block hizi accounts na tovuti, mfano kama mtu tu akimkashifu RAIS, namba yake itafuatiliwa mpaka apatikane, vipi ishindikane kwa hawa.
Media na vyombo vya habari ni kama vimekaa kimya na wakati wenyewe ndio wadau wa kwanza kwenye mitandao ya kijamii na wakiwa na wafuasi wengi. Wangetumia platform zao kufikisha elimu kwa watu wote. bila kuchoka maana tunakoelea sio kuzuri.
NAOMBA HILI CHAPISHO LANGU LIWE SHARED ZAIDI NA ZAIDI NA WADAU WENGINE WA MAENDELEO NA WENYE NIA NZURI WAWEZE KUTOA ELIMU ZAIDI JUU YA HILI TATIZO. ASANTENI

Upvote
0