FREEMAN MBOE
Kwa viongozi wote wa Baraza la Wazee na Baraza la Vijana waliochaguliwa, hongereni kwa ushindi wenu! Bidii yenu katika harakati zetu imekuwa msingi wa mafanikio haya, inayowapa fursa ya kuwa viongozi wa kuonyesha njia kwa wengine katika kuongoza Baraza lenu. Kwa wale ambao hawakushinda mara hii, juhudi zenu zina thamani kubwa kwetu na mnabaki kuwa nguzo muhimu katika safari yetu. Tunapoangalia mbele kuelekea uchaguzi wa ndani wa Baraza la Wanawake, nawatakia kina mama wetu heri ya kufanikiwa na wepesi katika kukamilisha jukumu hili muhimu. Kumbukeni, we are Stronger Together katika kufanikisha harakati zetu za kutafuta Tanzania bora, na sasa zaidi kuliko wakati wowote, tunahitajiana. Tuendelee kujenga chama chetu kwa umoja, upendo na moyo wa ujasiri, ili pamoja, tuweze kufikia ndoto zetu.
VS
Tundu Antiphas Lissu @TunduALissu
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa BAWACHA. Kama unataka na wewe, au mwanamke mwenzako anayefaa nae apate fursa za uongozi bungeni au kwenye udiwani miaka ijayo, nakushauri upige kura ya mabadiliko kwenye Uchaguzi wa BAWACHA kesho na Uchaguzi Mkuu wa chama tarehe 21 Januari.
Ni kura ya mabadiliko pekee itakayoondoa umalkia katika ubunge na udiwani wa viti maalum katika chama chetu. Ni kura ya mabadiliko pekee itakayohakikisha wanawake wengine nao wanapata fursa za kuwa wabunge na madiwani wa viti maalum.
Celestine Malley-Simba ameweka msimamo wake wazi kwamba atapiga kura ya mabadiliko tarehe 21 Januari. Na mimi namuunga mkono; lakini mimi sio mpiga kura kesho, na wala viti maalum havinifaidishi mimi binafsi.
Wewe uliye mpiga kura wa BAWACHA kesho na viti maalum vya ubunge na udiwani vinakuhusu, nenda kaunge mkono mabadiliko ndani ya chama chetu. Piga kura yako kwa Celestine Malley-Simba kuwa Mwenyekiti wa BAWACHA.
PIMA NANI KIONGOZI NA NANI MGAWA CHAMA