Somali Pirates Hijack Ship with 20 Americans!

wamarekani wana mzuka wa ugomvi,pili wanapenda kufanya matukio ya kuwa hero,kwakuwa watu wengi walikamatwa na pesa ikalipwa,hapo wao watataka kuonyesha kwamba wao hela hawana ila ubavu wanao.ingekuwa wamepandisha nae adundani kwao ningesema pana majadiliano lakini wako ndani ya boat iliyoishiwa mafuta tena mbele ya meli ya kivita ambayo inazana zote,hapo wasomali wanatafuta njia ya kuwaambia jamaa zao jinsi ya kulea watoto wao,maana hapo kutoka tena hakuna,na huyo bw barrack kashaonekana ykhe yakhe sasa nae atataka kuonesha si mdebwedo ni ngangari.duuu masikini mogadishu kuna msbamziiito vijana wanne watakufa punde,kalu ina lilah wainailaih rajiun,
 
...duuu masikini mogadishu kuna msbamziiito vijana wanne watakufa punde,kalu ina lilah wainailaih rajiun,

...yakhe waihadithia kama mpira vile 😀😀😀 roho za watu watano zi mashakani hapo... ilobakia jamaa washahadie wakijiandaa kukutana na muumba wao! ...hiyo cat-and-mouse inayoendelea sasa ni kuwachosha akili na njaa tu hao maharamia, baada ya masaa machache hadithi itakuwa nyingine...!

 
tunahitaj sampuli ya wasomali waje watusaidie issue ya kuibiwa samak pwan yetu
 
..mnh 🙁 kaazi kweli kweli huu mtanange !!!


...huenda soon pakatokea 'vita' vya maana huko kwenye pwani ya Afrika mashariki baina wa wasomali na meli zao dhidi ya wamarekani na manowari zao, hii kujitolea mhanga kunawapa bichwa sana hawa!
 
tunahitaj sampuli ya wasomali waje watusaidie issue ya kuibiwa samak pwan yetu

...wala usiombee hayo mkubwa, hukumbuki walivyosumbua kule Ngorongoro miaka ile mpaka serikali ya Ali Hassan Mwinyi wakapeleka majeshi?
 
unapokuwa na nchi ambayo haina control.......matokeo yake ndio haya.......hii ni hatari kwa nchi zote zinazotumia huduma ya meli.......iwe direct or indirect.....
 
Na inavyoonyesha hao wasomali/pirates walipenda kuvuna vya bure(ransom) wakati Marekani kisheria hakuna hela ya burebure hutolewa kwneda kwa pirates hivyo lazima kieleweke,kumbukeni hata waziri wa mambo ya inje wa Somalia alisema hapo pirates wameshika pabaya"they are playing with fire"
 
huyo waziri nae kujipendekeza tuu,kwanini serikali yaoisiwashughulikie hao maharamia.lakini biden alisema obama wa mtest ndani ya miezi sita,sasa kama hakutia kitimtim watamuona aaah yule ndo walewale wa kwetu askari anakuja barazani anasema salamalykum na anauliza shehe jumbe yuko wapi anajibu mimi, na askari anasema shehe nimetumwa na wakubwa nije nkutie mbaroni.hapotifu litamwagika.wewe unaona wanaongeza meli zengine!!!! sasa meli zote kwa ajili ya watu wanne tu au wanataka kusafisha pwani yote??? tobaaaa!!!! ndugu zetu kilioni.
 
Wajua US wameamua peleka mimeli yote hiyo japo kuonyesha kila mumarekani mahali popote alipo analindwa kwa nguvu zote na pia ni kuudhibitishia ulimwengu kuwa hata kama ni mtoto mdogo wa Kimarekani atalindwa kwa nguvu zote kama ilivyo Israel.Kuhusu Somalia Government=unfunctionable,hakuna serikali pale kuna watu wanakula posho za bure,wale jamaa(pirates) wana serikali yao ya kiharamia ndani ya somalia na jamaa ni wabaya kulikoni kuna tetesi kuwa huwa hawajui kama watu hulala usingizi wao macho kavu 24hrs=milungi kwa kwenda mbele!!.Lakini hapa ofcourse wamegusa pabaya ngoja kwanza wapate kichapo na pia wasambalatishwe ili kuwe na amani hiyo sehemu ili watu wafanye biashra zao halali.
 
...habari zenda zikijiongeza;


...Norweigians wao uzalendo umewashinda, wametoa dau;

 
Napendekeza operation kali ifanyike hapo Somalia hawa jamaa ikiwezekana wote watiwe nguvuni ili liwe fundisho,inatuasili sana kibiashara,unaweza agiza gari toka UK ukashangaa meli imetekwa na haya makenge,njaa zao wazipeleke somalia hukohuko si kwingine,noma sana,inauma!
 
Wanajf hivi hawa maharamia wa kisomali wanazo nguvu kiasi gani cha kuweza kutikisa hii ghuba??

Je wanashirikiana na watu wa Mataifa mengine kufanya hii biashara ya utekaji wa Meli za mizigo kwenye hii ghuba??

Kama nchi za magharibi zimeweka meli za kijeshi kwenye hii ghuba kitu gani kinawapa hawa maharamia kiburi cha kuendela na hii biashara??

Je silaha wanazotumia wanazipata wapi?? na vyombo wanavyotumia katika uporaji je ni ubora gani kulinganisha na za majeshi ya nchi za kigeni kwenye Pwani hii??
 
Je wanateka Meli zinazotoka nje ya Africa kwenda Afrika au wao wanateka Meli yoyote ile wanayoiona??
 
Je wanateka Meli zinazotoka nje ya Africa kwenda Afrika au wao wanateka Meli yoyote ile wanayoiona??

...meli yoyote ya kiraia inayoelea halali yao...!

Wanajf hivi hawa maharamia wa kisomali wanazo nguvu kiasi gani cha kuweza kutikisa hii ghuba??

...nia tu rohoni, si unajua tena they've got nothing to lose!

Je wanashirikiana na watu wa Mataifa mengine kufanya hii biashara ya utekaji wa Meli za mizigo kwenye hii ghuba??

...hawamtegemei mtu hawa, wenyewe kina 'Worya!' , hawana hata nchi hawa!

Kama nchi za magharibi zimeweka meli za kijeshi kwenye ni ghuba kitu gani kinawapa hawa maharamia kiburi cha kuendela na hii biashara??

...wakimteka raia mmoja wa kigeni, thamani ya kumwachia si chini ya $2m!

Je silaha wanazotumia wanazipata wapi?? na vyombo wanavyotumia katika uporaji je ni ubora gani kulinganisha na za majeshi ya nchi za kigeni kwenye Pwani hii??

...AK-47, na RPG's,...silaha za miaka na miaka za vita vya wenyewe kwa wenyewe,..na silaha mpya wanazonunua baada ya kupokea hizo ransom, na hizo boat zao zenye engine si chini ya 135mph


...'ukitaka kuua nyuki inabidi ulichome sega lote badala ya kuua nyuki mmoja mmoja', kwa maana hiyo unaonaje kijiji na miji yao yote ikaangamizwa? hutapiga kelele za inhumanity?
 
Mkuu Mbu katika usomaji wangu wa habari za hawa watekaji mara nyingi nimeona wanate Meli zilizotoka/zinazotka nje ya Afrika, nikawa ninajiuliza kama wao wanatarget zaidi meli ambazo zina shehena muhimu kwa Waafrika zaidi ya bidhaa kutoka Afrika. au habari za upande wa pili haziandikwi na vyombo vya habari.
Na ukiangalia kama hii meli ya mwisho kutekwa ilikuwa zaidi ya maili 300 toka pwani Mombasa, kwa maana hiyo nadhani wabahari wa hizi Meli yawezekana kama wanakauzembe fulani.
 
Bad rules when noble people do nothing.
Kwanza kabisa suala ili lisifumbuwe macho kabisa.
Wasomali serikali yao imesambaratika, iliyopo ni ya kiharamia.
Jumuia ya kimataifa ni lazima iweke agenda rasmi ya kutambua na kujenga mkakati wa kutatua tatizo la Somalia.
Somalia kama nchi kamwe haiwezi kwenda popote kwa kweka kitega uchumi katika mradi huu wa kuteka meli.
Hadithi zilizo achwa na waasisi wa Upirate duniani zinatisha, Wasomali hawawezi kuepuka jinamizi la Uharamia huu.

Fedha watapata na uhasama mkubwa kabisa utajengwa kuanzia Saudia hadi Ulaya, China hadi Marekani na Urusi hadi Asia ya kusini. Sioni ni vuipi mradi huu utadumu.

Nchi zote Duniani zinaona kama vile tatizo la kutekwa meli ni la wenye meli si tatizo la kimataifa.
KWa vile tatizo haliko baharini balini nchi kavu ndani ya Somalia, Ili kumaliza ngebe na kung'oa mzizi wa utekaji nyala meli ni lazima tena kwenda ndani ya Somalia. Sivyo Waweke No sailing Zone, mtu akiingia kwenye hizo 18 kusiwe na lawama.
Sivyo Arm kila meli inayopita hapo.
 
...Na ukiangalia kama hii meli ya mwisho kutekwa ilikuwa zaidi ya maili 300 toka pwani Mombasa, kwa maana hiyo nadhani wabahari wa hizi Meli yawezekana kama wanakauzembe fulani.

...hapana Mtu wa Kawaida, maritime procedures zinawataka;
" Crews not to resist pirates. Company practice is for all officers to go into safe rooms on board their ships and 'not to take on or actively engage.' "

Kwa maana hiyo, wale mabaharia wa kimarekani walojikomboa wamevunja sheria!

 

...International relations at stake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…