somali pirates
upandacho ndio uvunacho,ukipanda uovu utavuna uovu,mimi ninalaani vitendo vya kiharamia vinavyo fanywa na wasomali kunyangaya meli zinazo pita njia,katika dunia hakuna hata dini moja inayoruhusu mtu kumyanganya mwenzake mali yake, dini zote zinatutaka tuishi kwa salama na amani,takriban miaka 16 wasomali walikua wanatoana roho kama hawana akili vizuri,mwaka juzi wakatokea mmoja wao akashida wenzake akakamata madaraka na alhamdulillahi tulisikia sote duniani kwamba sasa unalala mlango nje hakuna jambazi wala kibaka,alie subutu kuvunja amri na kuanzisha fujo,kusikia hivyo tu mmarekani akapeleka vibaraka wake wahabeshi wende wakaiondoe ile serikali iliyoleta amani,lengo la mmarekani kuwatuma wahabeshi kwenda kuiondoa ile serikali ya amani anaijua mwenyewe na kweli waliiondoa ile amani na kurudisha balaa ambayo sasa hivi na wao wanalionja joto la jiwe,ukimuombea jirani yako amani Mungu kwanza anakupa wewe hio amani,na ukipanda mwanzi usitegemee kuvuna muwa wa sukari