Somalia: Al Shabaab yashambulia kambi ya wanajeshi wa AU

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Kundi la Al Shabaab la Somalia limeshambulia kambi ya wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AU) katika Mkoa wa Shabelle katikati mwa nchi hiyo, ikidaiwa raia watatu wamepoteza maisha katika mapigano hayo.

Mkazi mmoja anayeishi katika kijiji kilicho karibu na eneo la tukio, alisema baadaye aliona helikopta mbili zikipita na milio ya risasi ikitoka kwao.

Kamanda wa Jeshi wa Shaballe, Col Muse Hassan wapiganaji wa Al-Shabaab wakiwa na silaha nzito walishambulia katika nafasi tofauti. Walitumia gari lililokuwa na bomu likavunja geti ndipo wakaingia na kurushiana risasi kwa saa moja.

Al-Shabaab wamekiri kuhusika na kusema wameua wanajeshi 59 lakini mamlaka zimegoma kutoa idadi ya wanajeshi waliofariki.

Source: CNN
 
yaani huko unazaliwa mpaka unakufa ni milio tu ya risasi na mabomu
 
Alshabaab kuna siku watatwaa nchi kama alqaeda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…