Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Vitongoji vya makaazi karibu na Ikulu ya Rais wa Somalia mjini Mogadishu vimeshambuliwa kwa mabomu leo, muda mfupi baada ya Bunge la nchi hiyo kuidhinisha Baraza la Mawaziri lenye wajumbe 75 lililoteuliwa hivi karibuni chini ya Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre. Mamlaka zimesema hakuna majuruhi.
Tukio hilo linaonyesha wazi changamoto za usalama zitakazoikabili serikali mpya ya Rais Hassan Sheikh Mohamud, kutokana na uasi mkubwa wa makundi yenye itikadi kali za kiislamu, hasa kundi la Al-Shabaab ambalo limekuwa likifanya mashambulizi kadhaa katika miezi ya hivi karibuni.
Somalia, taifa lililopo katika pembe ya Afrika linakabiliwa pia na umasikini na janga la njaa.