Somalia: Watu 24 wafariki dunia baada ya boti kupinduka Bahari ya Hindi

Somalia: Watu 24 wafariki dunia baada ya boti kupinduka Bahari ya Hindi

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Takribani watu 24 wamefariki dunia baada ya boti mbili zilizokuwa zimebeba raia wa Somalia kupinduka katika pwani ya Madagascar.

Taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Somalia zinasema juhudi zinaendelea kuhakikisha kuwa manusura wanaokolewa wakiwa salama.

Boti hizo mbili zilikuwa zimebeba abiria 70 ziligunduliwa zikiwa karibu na pwani ya kaskazini mwa Madagascar Novemba 23, 2024 katika Bahari ya Hindi hata hivyo Inadaiwa sababu ya boti hizo kupinduka ni injini kufeli.

Walionusurika wanasema walikuwa safarini kwenda kisiwa cha Ufaransa cha Mayotte kwa wahamiaji wa Kisomali wanaotafuta hifadhi.

Madagascar imetoa onyo kali kuhusu uhamiaji haramu na kusema waathirika wa janga hilo walikuwa wahamiaji.

Sma pia: Warembo wawili wa Brazil wafariki baada ya kukataa kuvaa Jaketi za Kuokoa Maisha ili kupiga Selfies katika ajali ya Boti

Screenshot 2024-11-25 102813.png

Chanzo: Mwananchi
 
Wapumzike kwa amani sana Mama bikira Maria awaombee

Huenda walikuwa wanakimbia janga kubwa la uislam waende wakajihifadhi kwenye nchi za kikristo ili wapate tulizo la moyo
 
Back
Top Bottom