Its Pancho
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 15,966
- 26,404
Mara nyingi nimekuwa mtu wa mizaha hapa jamvini .
Ila basi baada ya kushuhudia kisa Fulani mtaani ,nikaona nishee kidogo nanyi kuhusu maisha yangu ya mahusiano kidogo huenda tukapata kitu hapa.
Well ,
Nikiwa na miaka 16 tu na nimemaliza kidato cha nne that time.mwaka Fulani.
Na kupata ufaulu wa kuridhisha wazazi walinitaka kwenda kusoma A level haraka sana..
Lakini hayo hayakuwa kichwani ,sikutaka kusoma tena ,akili yangu iliwaza kujichanganya mtaani na kupiga mishe na washkaji..
Kama mjuavyo ujana maji ya moto, katika kuruka ruka ,nikampa ujauzito binti mmoja niliyemzidi mwaka na darasa moja alikuwa kidato cha tatu, hapo ntyuka secondary.
Na kipindi hicho tayari sikuwa nakaa home japo nilikuwa gheto ila ni mtaani hapo hapo.
Well, binti huyo tumpe jina amina, kwao baba yake alikuwa ni fundi viatu, hivyo maisha yalikuwa ya kipato cha kati,
Wazazi wake hawakumuelewa kabisa kuhusu ujauzito, kama mjuavyo nisingeweza itelekeza damu yangu kwa kuchoropoa mimba..never
Nikajitokeza kwao ,mzee wake amina aliwaka sana kiasi cha kunikunja shati, kwani huyo alikuwa mtoto wao pekee alikuwa anasoma na walitegemea awavushe kwenye umaskini ,niliumia lakini maji nilishayavulia nguo ,
Tayari nilikuwa nlikuwa nna miaka 17 mwaka ulipita..
Huku nyumbani wakiwa wanajua kuwa sasa huko gheto nimeoa na Mara nyingi nilipokuwa nimekwama mama alinisaidia ,kwani mshua yeye nilimuonea jau kutokana na kutokumsikiliza ushauri wake (niendelee kusoma)
Nilikuwa dj mkali mtaani ninaefahamika,tenda nilipata nyingi ,
Washkaji niliokuwa nao gheto walikuwa wanakula kupitia Mimi.
Ila baada ya kuoa nikawatimua na nikaanza safari ya maisha rasmi huku nikipata mtoto mmoja wa kiume tumuite peter..
Mama peter akiwa na miaka 17 Mimi nikiwa na 18 na siku kadhaa( kwani nimezaliwa mwezi wa 12)
Baada tu ya yeye kujifungua, huko kwao aliporudi akawa hafanyi kazi kuwa bado ana kidonda ,huwa sifatilii hayo.
Nikawa nachota maji na napika then naingia mzigoni nilipata kazi redio moja hapo mjini ..
kama mjuavyo Dada zangu nyumbani (mawifi hawaishi kumsema kuwa ni mvivu )
Wakaniambia nichunguze na nimnyooshe, ila nikajua mke wangu bado hajapona atakaa sawa.
Mtoto alipoanza kutembea, yeye mama peter safari za kwenda kwao zikawa haziishi , na kumbuka kufika kwao ni kama mitaa mitatu tu..!
Akienda kwao anakaa wiki mbili, akirudi nyumbani anakaa siku tatu anarudi kwao..
Nikajua huyu atakuwa na home sickness.. Nikawa napita kwao naacha pesa hata ya mboga, kumcheki mwanangu, naondoka kulala kwangu..
Mtu atakunyima chakula lakini sio maneno..!
Ndio, nilianza kuskia maneno kitaani kwa watu kuwa nimeoa mke cha wote ,sijui anagawa mbele na nyuma.!
Nikapuuzia..
Ila baada ya muda safari za kwao zikawa too much kwa kweli .
Anaweza kwenda kwao kushinda huko jioni anageuza..!
Unapochagua boga penda na ua lake
Nilimpenda kuliko watu wote niliowahi kuwa nao, vyovyote niliamua kutulia nae .
Lakini yeye kumbe bado alikuwa kwenye foolish age.!
Hakutakiwa kuwa kwenye ndoa hapo hata Mimi pia lakini experience ilinibadilisha na kunikomaza.
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza..!
Wahenga hawakukosea msemo huu
Siku hiyo naondoka nyumbani mchana na kumuaga mama peter naelekea kazini kwani nilikuwa nna kipindi mchana, nae akaaga atakuwa kwao.
Nipo zangu kwa daladala (kipindi hicho bajaj hazikufanya root town Dom)
Mshkaji mmoja tulisoma nae yupo kitaani ,akanichana "nimemuona shem anaingia gesti pale"
Nikajua tu maneno ya watu ila jamaa akanionesha na picha mbili alizopiga.!
Hapo akili ikaanza kuja,
Kwakuwa nilikuwa sijakomaa kiakili nikapanga kwenda eti kufumania..!
Nikamchukua mwamba mmoja wa kuitwa kuka mbavu Nene.
Tukaenda mpka gesti tajwa..ilikuwa mitaa ya hazina..
Naendelea tuwe hapa ..
Pancho boy