Hakuna kukata tamaa Mkuu ingawa chamoto lazima ukione.Matatizo ni sehemu ya maisha ya mwanadamu,
Na sometimes matatizo huja ili kutufunza ili next time tuwe makini zaidi,
Kinachotakiwa ni binadamu kutokukata tamaa na kukabiliana na hayo matatizo.
Sio unajipata unaanza kutamani wakina Giggy(reckless life).Amini nyakati ngumu hazidumu
usijifananishe wala Kujilinganisha na mwingine
Jaribu kufanya mambo mengine kama jambo unalofanya limegoma
Usisikilize sana maneno mtaani
Jifunze kwa wengine unaowaamini
Usikate tamaa, ukitaka kufahamu hili angalia ndege anavyotengeza kiota ndio utashangaa kutoka kajani kamoja hadi kuwa kiota sio mchezo.
ukijipata ishi kawaida kama ulivyozoea bajeti yako.
Inasikitisha sana!Hellow JF.
Unakuta.
Unajiheshimu/Umejitunza vizuri unakuja kuoa/olewa na Malaya sugu.
Umepambana umejinyima ukalima nyanya zako vizuri siku unaenda shambani nyanya zimeungua nusu shamba.
Umesoma vizuri mpaka chuo lakini hauoni fursa wala haupati ajira(kulala/kula yako ya shidashida). Upo kwa SHEMEJI YAKO NA JAMII INAKUSIMANGA KILA KUKICHA.
Umepanga fremu ya biashara mwaka unaisha hakuna ulichokipata mpaka unakosa kodi yakulipia tena Fremu.
Mshahara wako na majukumu yako vitu viwili tofauti kabisa(madeni kila kona) familia zina kutazama wewe kama mkombozi.
Umekomaa kwenye mafunzo ya ujeshi/polisi na umefanya vizuri kabisa lakini kila siku wanaitwa wengine hata ulio wazidi uwezo.
Wakuu sometimes ukilala hautamani kuamshwa kabisa.