The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 1,497
- 2,681
SOMO: ADUI MKUBWA WA NDOA
Kila ndoa ina taaabu zake.Hakuna ndoa yoyote duniani aambayo haina changamoto. LAKINI kuna Mambo yakipewa nafasi yanaweza kuleta balaa kwenye ndoa yoyote Ile .
Hapa tunaenda kuangalia Kwa undani adui huyu mkubwa n yupi!
1. ZINAA (KUTOKA NJE YA NDOA )
Kuhusu hili imeandikwa Kutoka 20:14 “Usizini.
Pia imeandikwa
Methali 5:15 Mkeo ni kama kisima cha maji safi: Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe.
Methali 5:16 Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali, na vijito vya maji barabarani?
Methali 5:17 Hiyo ni yako wewe mwenyewe, wala usiwashirikishe watu wengine.
Methali 5:18 Chemchemi yako na ibarikiwe, umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana.
(BHN)
Dhambi hii kwenye ndoa ndiyo dhambi mbaya sana kuzidi dhambi zote unazoweza kumfanyiwa mwenzi wako kwa sababu zifuatazo
1.Inavunja Amri ya Mungu Kutoka 20:14
2. Inawaunganisha kimwili watu wawili wasiofaa kuunganishwa 1 kor 6:16
3. Huleta aibu na kuonekana kukosa akili Mithali 6:32
KWANINI WATU HUENDA KUTAFUTA NGONO NJE YA NDOA?? Hizi hapa sababu .
1. Kukosekana kwa ngono nyumbani kwake
2. Kufanya ngono isiyoridhisha kati ya wenzi wawili [Kutoka 21:10]
3. Kuendeleza mawasiliano ya wapenzi wa zamani aliokuwa nao kabla ya kuoa au kuolewa
4. Kujaribu nje kuona kama walioko nje wanafanana na yule aliyenaye
5. Kuwa na urafiki na wapenda ngono (wazinifu) 1 kor 15:33
6. Tabia ya mtu mwenyewe
7. Utamaduni wa watu fulani
8. Kama njia ya kumwadhibu mwenzake kwa kosa fulani
9. Kulipiza kisasi baada ya mmoja kumsaliti mwenzake .
MATOKEO YA ZINAA KWENYE NDOA
1. Kifo cha kiroho
2. Kuteseka kwa aliyebaki kuwa mwaminifu .
3. Kupata magonjwa ya zinaa
4. Kuleta mbegu au mtoto asiyehitajika
5. Kuvunjika kwa ndoa
6. Kuuawa,kudhalilishwa ,kutiwa ulemavu wa kudumu endapo ukifumaniwa .
7. Kutelekeza familia
8. Kukosa uzima wa milele.
DAWA YA ZINAA.
1. Apate Ngono ya kutosha nyumbani kwake
2. Kila mmoja ajue wale wa nje hawana jipya mambo ni yale yale ..atosheke na aliyenaye
3. Mawasiliano yawepo ya kutosha yatakayopelekea ngono kutokauka nyumbani
4. Watafute namna ya kuwa karbu mara nyingi mwanzo 2:24, kama wana kazi za mikoa tofauti watafute uhamisho wakae eneo moja
5. Kila mmoja awe wazzi kwa mwenzake
1 Wakorintho 7:2 lakini kwa sababu ya hatari ya uzinzi, basi, kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
1 Wakorintho 7:3 Mume atimize wajibu alio nao kwa mkewe, naye mke atimize wajibu alio nao kwa mumewe.
1 Wakorintho 7:4 Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe anayo; hali kadhalika naye mume, hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mkewe anayo.
1 Wakorintho 7:5 Msinyimane haki zenu, isipokuwa kama mnaafikiana kufanya hivyo kwa kitambo tu, ili mpate nafasi nzuri ya kusali. Kisha rudianeni tena mara, ili Shetani asije akawajaribuni kwa sababu ya udhaifu wenu.
Mbarikiwe wajoli.