SOMO LA BURE: IPSAS Accruals based TZS.trilioni 1.5

article

Senior Member
Joined
Sep 10, 2016
Posts
186
Reaction score
344
UTANGULIZI.
Masuala yanayohusiana na uhasibu yanachukuliwa na watu wengi kwamba yanaboa au hayaeleweki kutokana na kuhusisha hesabu ambazo kwa upande wangu naweza kusema huwa hazifundishwi vizuri kwenye taasisi nyingi za kujifunzia na kupelekea hali hii.Uhasibu ni kitu nyeti sana hasa linapokuja suala la fedha za Umma ,biashara au suala lolote linalogusa pesa.

Nimeamua kuja na mada hii nikiwa kama mdau wa Elimu kwa Umma inayohusu masuala ya fedha ili angalau nitoe mwanga kidogo kwa wale ambao somo la fedha liliwapita mbali kidogo na kuwakumbushia kidogo wale wenye ufahamu ulioanza kufifia juu ya Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma vinavyotambua matarajio (IPSAS Accruals based.) ambavyo vinatumiwa kwa sasa na Taasisi za Umma nchini(zikijumuisha Halmashauri,Manispaaa,Majiji,Mashirika ya umma na Vyama vya siasa) kuandaa na kuwasilisha taarifa za fedha kwa Umma.
IPSAS Accruals based ni mfumo wa Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu katika Sekta ya Umma vinavyotambua matarajio ambao unatambua mapato yaliyopatikama na matumizi yaliyofanyika pindi muamala husika unapokamilika bila ya kujali kama fedha taslimu imepokelewa au matumizi kulipwa kwa fedha taslimu pia mfumo huu unahitaji uthaminishaji wa mali na madeni kuendana na wakati na hali ya kiuchumi kwa ujumla na kwa kipekee kwa taasissi husika.

Mfumo wa IPSAS Accruals based ili uweze kufanikiwa yafuatayo inababidi yazingatiwe:
  • Elimu ya kutosha itolewe kwa waandaaji wa taarifa za fedha na watumiaji hasa Mawaziri,Viongozi wa Juu Wizara ya fedha ,Wabunge,Jamii kwa ujumla na vyombo vya juu vya ukaguzi wa Hesabu za Serikali .Elimu inaweza kutolewa kwa njia mbalimbali zikiwemo mihadhara,njia za kielectroniki,vitini kuaandaa sehemu maalum ya kutoa elimu husika kwa anayehitaji.Elimu ya kutosha isipotolewa taarifa za fedha zitakazowasilishwa zinaweza zikatamfsiliwa vibaya na watumiajia au kutoeleweka vizuri hivyo kushindwa kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kutumia viwango husika kwa kuzua mijadala na malumbano yasiyoisha kwa watumiaji wa taarifa husika.

    Kwa mfano katika nchini yetu changamoto za uelewa wa IPSAS Accruals based zilijitokeza kwa upande wa baadhi ya watunga sheria na wadau wengine mbalimbali kuelewa taarifa za fedha za serikali zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali(CAG) kwa mwaka wa fedha 2016/2017zilizowasilishwa Bungeni.Taarifa husika ziliandaliwa na kuwasilishwa kwenye mfumo wa IPSAS Accruals based ambapo Naibu Waziri mwenye dhamana kwenye Wizara husika alilazimika kutoa ufafanuzi baada ya kuibuka kwa mjadala mzito wa kiasi cha TZS. trilioni 1.5 kilichoonekana kwenye taarifa na kudaiwa kutumika pasipo maelezo toshelezi.Akitoa ufafanunuzi Dk. Kijaji Naibu waziri mwenye dhamana alisema matokeo ya utekelezaji wa mfumo wa IPSAS Accruals based yameiwezesha serikali kutoa taarifa za uwazi katika taasisi zake na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa mipango.Alisema hakuna kiasi cha TZS. trilioni 1.5 kilichopotea au kutumika bila kuidhinishwa na Bunge, bali ni kutokana na serikali kutumia mfumo wa IPSAS Accrual.Baada ya ufafanuzi kutolewa baadhi ya watunga sheria walilidhika na ufafanuzi uliotolewa wengine walihitaji ufafanuzi zaidi juu ya suala hili kutoka kwa mamlaka za juu.
  • Kuwe na mpango kazi mzuri wa jinsi gani ya kuhamia kwenye mfumo huu kutoka kwenye mfumo wa zamani.Hili jambo lisipofanyika kwa umakini mkubwa mbele kuna uwezekano mkubwa mvurugano kutokea mbeleni.
  • Inapaswa Mfumo uungwe mkono kisiasa pia uungwe mkono viongozi wa njuu kwenye taasisi zote nyeti za Umma ili uweze kufanikiwa.
FAIDA KUU YA MFUMO WA IPSAS ACCRUALS BASED.

Uwazi wa hali ya juu,Ukweli na Uwajibikaji.

Mapato na Matumizi yote halali kwa ujumla wake yanaonyeshwa kwenye Taarifa za fedha bila ya kujali kama fedha taslimu imepokelewa au matumizi yamelipwa na mfumo unaitaji uthaminisha wa mali na madeni ili kuendana na wakati na hali ya kiuchumi kwa ujumla.

Mfano 1:
Matumizi.

Serikali X ilikuwa inadaiwa jumla ya USD.10 bilioni za Mishahara ya Watumishi wake kwa mwaka fedha 2017/2018 na ikaweza kulipa fedha taslimu USD. bilion 7
Kwa kutumia mfumo wa IPSAS Accruals based Taarifa ya mapato na matumizi (Statement of Income and Expenditure) kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ya Serikali X itaonyesha matumizi kwenye mishahara ya USD. bilioni 10 na siyo fedha taslimu USD. bilioni 7 ambazo zililipwa . Serikali hiyo kwa mwaka husika pia itaripoti kwenye Taarifa yake ya mizania iliyounganishwa(Consolidated Statement of financial Position) kiasi cha Deni la TZS. bilioni 3 kama Madeni ya Mishahara ya Watumishi .

Hivyo, Serikali X itakuwa imesema ukweli na kuweka wazi taarifa za mishahara ya Watumishi wake na itawajibika kulipa deni la mishahara ya Watumishi lililopo kwenye taarifa zake za fedha.

Mfano 2:
Mapato.

Serikali X ilikuwa inadai kodi halali USD. bilioni 15 kutoka kwa walipakodi wake kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na ikaweza kukusanya fedha taslimu USD. bilioni 10 za kodi husika. Kwa kutumia mfumo wa IPSAS Accruals based Taarifa ya mapato na matumizi (Statement of Income and Expenditure) kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ya Serikali X itaonyesha mapato ya kodi ya USD. bilioni 15 na siyo fedha taslimu USD.10 bilioni ambazo zilikusanya kutoka kwa walipakodi. Serikali hiyo kwa mwaka husika pia itaripoti kwenye Taarifa yake ya mizania iliyounganishwa(Consolidated Statement of financial Position) kiasi cha USD. bilioni 5 kama mapato tarajia(Receivables) kutoka kwenye kodi.

Hivyo, Serikali X itakuwa imesema ukweli na kuweka wazi taarifa za mapato yake ya kodi na itawajibika sasa kukusanya kiasi cha mapato ya kodi kisichokusanywa kilichopo kwenye taarifa zake za fedha kilichoripotiwa kama mapato tarajiwa ya kodi.

CHANGAMOTO KUU YA MFUMO WA IPSAS ACCRUALS BASED.
  • Taarifa za fedha zilizoandaliwa kwa kutumia mfumo wa IPSAS Accruals based zinahitaji kufanya makisio na kufanya maamuzi juu ya uthaminishaji wa mali na madeni wakati wa kufanya makato ya makisio ya uchakavu na kushuka kwa thamani kwa mali(Provisions for depreciation) au makato ya makisio ya madeni yanayohofiwa kutolipwa (Provisions for bad and doubtful debts).
  • IPSAS Accruals based inahitaji wataalamu wenye ujuzi wa kutosha wa uhasibu(CPAs) ambao Serikali nyingi zinanakuwa hazina wa kutosha au zinapokuwa nao hazikai nao kwa muda mrefu .
  • Kwa kuongezea taarifa za fedha kwenye IPSAS Accruals based bila shaka ni tata na ni ngumu kuzielewa na zinaitaji mafunzo ya kutosha ili kuweza kuwatafsilia watunga sheria na Wafanya maamuzi wanaotegemea taarifa zilizoandaliwa kwenye mfumo huu.
Naomba kuwasilisha,

Article.
 
tunataka maelezo yatolewe na CAG. siyo makanjanja na misukule ya Lumumba
 
Kwenye Ukaguzi wa mahesabu huwa kuna ushirikishaji! Je, wakati wa Ukaguzi wa hyo 1.5 hawakishirikisha, Kwa nini maelezo yalipishana.. Umeandika vzuri ila kuna maswali mengi
 
Mkuu wewe ni mhasibu au una idea tu ya uhasibu? Kama wewe ni mhasibu, hicho ulichokiongea kina tofauti gani na IAS 1 na hiyo IPSAS? Pia IFRS ina-require ku-measure and recognise elements za financial statements kwa kutumia accrual basis na wala sio cash basis. My problem with you is that I do not see any difference between IFRS and IPSAS according to your argument. Taja kitu kingine unique ambacho kipo kwenye IPSAS, hicho ulichokitaji/kiongelea mbona ndio treatment ya kawaida kulingana na IFRS.
 
Suala la kwamba mimi ni Mhasibu au siyo Mhasibu nadhani halina msingi wowote ni vizuri tukajikita kwenye mada husika. Ila kwa kukutoa wasiwasi wewe na wasomaji wengine ni kwamba nina elimu ya juu ya uhasibu ya kuelimisha inayotambulika na mamlaka husika inayosimamia uhasibu nchini.

Nakushauri kasome zaidi kuhusiana na viwango vya kimataifa vya uhasibu kwenye sekta ya Umma(IPSAS):IPSAS accruals based na IPSAS cash based ,Viwango vya kimataifa vya kuwasilisha taarifa za fedha (IFRSs) na Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu(IASs) ili uweze kutoa mchango wako kikamilifu kwenye uzi huu.

Nikukumbushe pia kwamba IPSAS karibia zote zimeundwa kutoka kwenye IFRSs na IASs lakini baadhi zimerekebishwa kidogo ili kukidhi mahitaji ya sekta ya Umma.

Sina suala jingine la kuongelea kuhusu IPSAS kwenye mada ya leo kwa kuwa lengo la mada yangu lilikuwa nikutoa mwanga mdogo kwa Umma juu ya IPSAS accruals based.
 
Acha kupanic. Ulichokiongea hapo mwanzo, mtu ambaye haujui uhasibu anaweza ku-assume labda hiyo ndio tofauti ambayo anaweza kuikuta mtu aliyesoma diploma in IPAS na aliyesoma CPA. So ulichokiongea hakina tofauti yoyote, so hakuna jipya lolote. Kama unataka kuongelea IPSAS ongea kitu ambacho ni tofauti, sio una sensitize kitu ambacho is so common. Ongea kitu unique. Sio unaongea vitu ambavyo hata mwenye degree ya uhasibu anavijua, I mean mhasibu yoyote wa kawaida anaijua hiyo treatment ya accrual basis na wala huitaji kuielewa IPSAS au sio mpaka usome IPSAS ndio ujue accrual basis.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…