KERO Somo la BUSINESS STUDIES lina upungufu mkubwa wa Walimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Serikali ilizindua mtaala mpya na ulioboreshwa wa mwaka 2023 ulioanza kutumika mwaka 2024 kwa baadhi ya shule na mwaka 2025 ulianza kutumika kwa shule zote za sekondari.

Katika mtaala huu mpya somo la BUSINESS STUDIES limekuwa ni somo la lazima kuanzia kidato cha kwanza mpaka kidato cha nne... Pamoja na somo hili kuwa la lazima lakini halijapewa umakini mkubwa sana kwani halina walimu kabisa wa kuweza kufundisha somo hili.

Shule nyingi somo hili linafundishwa na walimu wa masomo mengine kama vile PHYSICS, MATHEMATICS, CHEMISTRY, BIOLOGY, HISTORY, GEOGRAPHY KISWAHILI, CIVICS.. Kwahiyo somo hili linafundishwa na walimu ambao siyo wabobezi katika maudhui ya kibiashara...

Hata walimu walioajiriwa hivi karibuni kwenda kufundisha somo hili wamekuta somo hili linafundishwa na walimu ambao siyo wabobezi katika somo hili... Hata kwenye baadhi ya shule ambazo walimu walioajiriwa kufundisha somo hili hususan wale waliosoma BACHELOR OF BUSINESS ADMINISTRATION imeonekana bado hawamudu kufundisha somo hili kwani wanafunzi wengi wanalalamika kutowaelewa walimu hao...

Rai yangu kwa Serikali - iliangalie mbali sana kutaka mtaala huu uanze kutumika mapema sana basi haina budi iajiri walimu wanaokidhi matakwa ili waweze kutusaidia kufundisha somo hili la BUSINESS STUDIES kwani kuna walimu wengi sana waliosoma masomo ya ECONOMICS na COMMERCE na wanamudu kufundisha somo hili la BUSINESS STUDIES. Mfano mdogo tu BETHELEHEMU SECONDARY SCHOOL iliyopo MBINGA TC somo hili linafundishwa na mwalimu mbobezi wa HISTORY....
 
Pole saana ndugu MWALIMU najua unatetea somo lako ili na wewe uajiriwe kama binadamu nakuelewa unachopitia binafsi ni nilikuwa na mwanamke ni mwalimu Wa phy na chem alimaliza chuo mwaka 2020 akiwa na GPA ya 4.6

Shule ya kwanza alifundisha wakawa wanamlipa laki 3

Shule ya pili wakawa wanamlipa laki 5 (hapa alikaa mwaka mmoja)

Then akapata shule ya Roman akawa analipwa laki 9 (hapa kwa miaka 3 mfululizo alikuwa anaongoza kufaulisha phy kimkoa)

Binafsi sikuridhika kuona kipenzi changu mtaalamu wa phy na chem analipwa laki 9 tu hivyo basi nilianzisha mpango mkakati wa majungu fitina na mbinu zote kumtoa kwenye ualimu mpaka kumpenyeza kwenye mamlaka moja na kuwa mkuu Wa dawati la Rasilimali watu

Moja ya mkakati niliofanya ni kumshawishi kigogo mmoja kuwa walimu wanatweza kuwa Ma HR na maafisa mahusiano wazuri akaingia huu mkenge akamtoa kipenzi changu kutoka privet mpaka kuwa mwalimu Wa gavoo na baada ya muda akamtoa kwenye ualimu mpaka huko kwenye mamlaka hiyo
Kwann nimekuadithia hiyo story
Jibu ni kuwa ndugu MWALIMU unapita mulemule ila unakosea kutaka taasisi za watu kwann usingesema Kuna shule moja mkoa fulani mpaka uitaje Jina
Huoni kuwa unahatarisha biashara ya watu

B
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…