Somo la dawa ya madoa

Beeb

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2018
Posts
29,394
Reaction score
59,069
Dawa ya kuondoa madoa kwenye nguo

MALIGHAFI

-Chloride acid(cassium hyperchlorite) robo kilo
-maji masafi lita10
-ndoo au pipa
-mwiko mrefu au mti mnene wa kukorogea

JINSI YA KUTENGENEZA
-andaa ndoo au pipa lako hakikisha ni safi na kavu
-weka maji Lita 10 kwenye ndoo au pipa lako
-weka chloride acid(cassium hyperchlorite)
-koroga kwa dakika 15 kisha acha itulie kwa muda wa masaa 8
-baada ya hapo utaona imejitenga uchafu kama jivu utakua chini maji yatakua juu
-engua maji juu ya juu ambayo ndio dawa ya madoa yenyewe pakia na ukauze

Nimeona tushirikishane vile ninavyovijua...najua kwa namna moja au nyingine nitakua nimesaidia.

Kama kuna sehemu haujaelewa kua huru kuuliza

Niwatakie mchana mwema
 
Nilisha wai tumia Jik kutoa madoa kwenye shati langu jeupe af maji yale yale nikafulia majinsi yangu. aiseee yalichanika yote. nilishinda bukta mwezi mzima
Hahahaha nimecheka....nini kilikusibu jiki kuweka kwenye jinsi?

Pole
 
Write -Chloride acid(cassium hyperchlorite) reply... hii inapatikana wap na beiyake pia
 
Thread Nzuri Sana Ila Avatar Ni Zaidi Kwa Uzuri 😂😘👏👌
 
Maduka ya malighafi za viwandani
Nataka kujua ni maduka gani hayo, pembejeo, maduka ya dawa baridi, au maduka ya ujenzi au wapi hasa??
 
Kwa Arusha sifahamu mkuu
Jamani, mara kwanza kuyasikia yanapatikana maeneo yote au ni sehemu maalum nishauri kwa Arusha naweza kupata wapi??
 
Nilisha wai tumia Jik kutoa madoa kwenye shati langu jeupe af maji yale yale nikafulia majinsi yangu. aiseee yalichanika yote. nilishinda bukta mwezi mzima
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Lowekea water guard kwa masaa machache then fua.. huo mlolongo wa kwenda viwandani ni mrefu, sana sana utaambiwa unatafuta malighafi za kutengeneza milipuko
 
Amekuelewa
Lowekea water guard kwa masaa machache then fua.. huo mlolongo wa kwenda viwandani ni mrefu, sana sana utaambiwa unatafuta malighafi za kutengeneza milipuko
 
Sahihi ni Calcium Hypochlorite.


Pia waweza tumia Sodium Hypochlorite
 
Naweka kambi hapa


Sent from my TECNO CG7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…