lugoda12
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 276
- 574
SOMO LA KEMIA KANISANI
WIVU + TAMAA X UJINGA WA MAMLAKA = burudani mitandaoni.
1. Kuna watu wamepigwa na kuumizwa, wasizuiwe kulia.
2. Kuna watu hawajui chanzo, wasizuiwe kuhoji hoji.
3. Kuna watu wanaujua ukweli wote; mitandao si mahali pa kuusemea.
4. Kuna watu wamekosea njia; wametibu dalili badala ya ugonjwa. Ni wakati wa kujifunza - si kufafanua wala kujitetea.
5. Kuna watu wanataka huruma; ni haki kuhurumiwa ukiumizwa lakini huruma ya binadamu haitoshi na haiponyi.
6. Kuna watu wanashangilia. Ni sawa na ngedere wachanga wachekao msitu unaoteketea wasijue jioni watalala wapi. Shoka lipo shinani…
7. Tunaona nini?
- Mti mbichi? Mkavu utakuwaje?
-Mchungaji apigwaye ili kutawanya kondoo?
-Ng’ombe aliyevunjwa mguu ili arejee zizini?
-Mfalme katili anayefukuza giza kwa kuzima mshumaa?
-Mtoto mkaidi asiyefaidi mpaka siku ya Idd?
-Baba mjinga anayekerwa na nyota ya jirani kuliko giza la nyumbani kwake?
Kuna kitu hakiko sawa mahali.
Tunahubiria wengine MARIDHIANO. Sasa turidhiane sisi. Baba Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza!