Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
MAMBO YA KUFIKRIKA YALIYOPO DUNIANI NI YAPI?
Kuna mambo mengi sana ya kufikirika yameundwa na kupewa uhai ambayo yanaleta ugomvi mwingi kwa watu hapa duniani. Katika masomo yangu haya niliyoyaanzisha ya kujitambua, kuna watu watajifunza na kufunguliwa nafsi zao na kuwa huru.Baadhi ya mambo ya Kufikirika Ni kama ifuatavyo:-
- Mungu
- Shetani
- Vyama vya Siasa
- Demokrasia
- Timu za mpira
- Mapenzi
- Nchi
- Kabila
Vitu hivi ni vya kufikirika havipo. Vimetengenezwa ndani ya ubongo tu.
Ili kuweza kujitambua, ni vyema kujua kuwa hayo mambo na mengine yafananayo na hayo ni vitu vya dhahania tu. Havina uwezo wa kujitetea maana havipo.
TUFANYEJE KUONDOKANA NA UTUMWA HUU WA KIFIRA
Ni muhimu sana kujenga tabia ya kujitazama kwenye kioo na kupata muda wa kukaa pekee yako. Kupata muda wa kuweza kufanya Meditation. Kufanya hivyo utaanza kujitambua wewe ni nani na uwezo wako upo namna gani.Baada ya kufunguliwa kutoka kwenye utumwa wa fikira utaanza kuwapenda binadamu wenzako. Hutaendeshwa na vitu vya kufikirika. Utaelewa wewe ni nani na lengo lako la kuwepo hapa ni nini.