NANDERA
JF-Expert Member
- Mar 18, 2014
- 2,024
- 2,487
Hebu tujadili pengo lililopo kati ya mitaala na ufundishaji halisi. Mwanangu yuko la pili. Daftari lake la stadi za kazi limejaa notes juu ya namna ya kutengeneza vitu mbalimbali. Leo kasoma somo la jinsi ya kutengeneza "twill band" (ukili). Akanakili hatua sita hivi, kisha ikafuatiwa na maswali.
1. taja vitu vitano vinavyohitajika kutengeza ukili
2. taja vitu vitano vinavyoweza kutengenezwa kwa ukili.
3. chora vitu vifuatavyo: kofia, kawa, mkeka na kikapu.
Mada ikaishia hapo, wiki ijayo wanaanza mada mpya. Mwisho wa muhula anafanya mtihani. Alivyo mzuri kukariri si ajabu akapata mia kwa mia mtoto wa watu. Stadi za kazi 100%!!
Sasa hii ndo nia ya huu mtaala? Nawaza mpaka nachoka. Saa nyingine nalazimika kuingia madukani kutafuta vitu tujaribu wenyewe nyumbani. Kwa mfano aina za rangi. Ilibidi nikazitafute baada ya kuona mtoto anatakiwa kukariri "ukichanganya rangi nyekundu na njano utapata rangi gani?
Kuna wakati nalaumu shule. Ada yote nayolipa wanashindwa nini kununua vitu vya muhimu wawafundishe watoto kwa vitendo? Au basi watuambie wazazi tununue? Nikakaa nikafikiria - hivi hata wakipeleka huyo mwalimu atakuwa na vipaji vingapi maana mtaala una mada nyingi mpaka mitindo ya kushona. Nikakumbuka enzi zetu hakukuwa na mtaala unaomfunga mwalimu. Mwalimu wa sanaa alikuwa anaagiza kila mwanafunzi akatengeneze kitu anachopenda na anachoweza. Mimi nilikuwa nikipeleka ngata tu maana ndo niliyoweza kumuiga bibi akitengeneza. Sikuwa na kipaji cha mikono bali cha maneno - kuandika na kuongea. Wenzangu walikuwa wakipeleka vitu walivyofuma, walivyochonga, walivyochora n.k. Kisha vilishindanishwa na aliyebuni vizuri alipewa zawadi na vitu vyao vikawa vinapamba ofisi ya walimu. Ilikuwa ni fahari kwa mwanafunzi husika.
Sasa huu mtindo wa kukaririsha watoto woooote kuchora, kusuka, kudarizi, mara do re mi fa so lati doooo!!!! yaani jamani ni majanga. Watoto wenyewe darasani hawazidi hata 20! Ingekuwa "kayumba" ningesema mazingira magumu.
Nimewahi kuona ITV shule flani flani zimeajiri walimu wa kudumu au wa kukodishwa wa sanaa, ambapo watoto hugawanywa kulingana na vipaji vyao kisha hufundishwa na kushindanishwa na kutuzwa. Yaani vipaji vyao vinakuzwa vizuri. Kuna wabunifu wa mitindo, wachoraji, waimbaji, wapiga vyombo n.k. Hela ya kumlipia ada shule hizo sina, lakini ningependa nimsaidie mwanangu kutafuta kipaji chake na kukikuza na kumfunza kazi za mikono kama kufuma, kushona na kusuka maana ni muhimu. Nifanyeje?
Funga kazi iko kwenye daftari la haiba na michezo (personality and sports development). Anaandika na kuchora michezo mbalimbali lakini ukimuuliza "mlicheza huu mchezo?" anakwambia "hapana. Tumeandika tu."!! Jamani hata mchezo wa dama na kuruka kamba mwalimu hawezi kusimamia watoto wacheze wenyewe??? Wanaandika notes ili iweje? Hili naenda kuongea na mkuu wa shule maana linaweza kutekelezeka ndani ya siku 2 akiamua. Nimevumilia sasa nimechoka. Walimu gani hawawezi kujiongeza jamani??? Najua ni matokeo ya mfumo lakini mbona shule zingine na walimu wengine wanajiongeza? Kwani wao wamekulia na kusoma wapi?