SOMO:Wanawake Pia Wana Upungufu Wa Nguvu Za Kike Pia

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,699
Reaction score
4,117
Mzunguko wa tendo zima la ndoa huwa umegawanyika katika nadharia kuu nne ambazo kwa lugha ya kiingreza huitwa excitement (kusisimka),plateu,orgasim (kilele) na resolution (kurudi katika hali ya kawaida).Hatua hizi siyo lengo letu kuzizungumzia kwenye post hii,tutaziona kwenye post inayokuja hivyo endelea kufuatilia page hii.Wanaume ni wahanga wa nguvu za kiume,lakini wanawake wengi pia hukumbwa au wamekuwa wanaishi na matatizo makubwa katika mojawapo ya hatua hizi (pengine hatua zote)

WANAATHIRIKA VIPI?
Mgawanyiko wa hatua nne tulizozitaja hapo juu tunaweza kuugawa pia katika makundi madogo manne
1.Kukosa hamu ya tendo la ndoa kunakoweza kusababishwa na mabadiliko ya homoni,magonjwa na matumizi ya aina fulani ya madawa,stress,mzio,ujauzito na kushiriki tendo hili kila muda
.
.
2.Kutokuwa na uwezo wa kusisimka (kusisimliwa) ambako huambatana na kutokuzalishwa au kuzalishwa kwa majimaji na ute mdogo kutokana na wasiwasi au kutokusisimliwa sana.Tafiti zinaendelea kufanyika juu ya namna gani msukumo wa damu kwenye uke huchangia kusisimka kwa hisia za mwanamke
.
.
3.Kutokufika kileleni ambako kunaweza kusababishwa na matatizo ya kiafya yanayoleta ugumu katika kufika kileleni,upungufu wa ujuzi na maarifa,kutokujijali (kufikiria kumridhisha sana mwanamme kuliko wewe mwenyewe) pamoja na matatizo ya kisaikolojia hasa wasiwasi,uoga na historia au kumbukumbu ya kunyanyaswa kingono
.
.
4.Maumivu wakati wa tendo la ndoa yanayosababishwa na matatizo hasa endometriosis,ovarian cysts,maambukizi ya uke,kukakamaa sana kwa misuli ya njia ya uke (vaginismus),kutokuzalishwa na ute na majimaji mengi pamoja na mambo mengine

Mambo haya hayasemwi sana lakini yanasumbua sana wanawake pengine kuzidi hata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume.Kuna baadhi ya wanawake pamoja na kuishi kwenye ndoa kwa miaka mingi hawajui kufika kileleni kupoje zaidi ya kuhisi tu bila kuifikia hali hii.Kama unapitia changamoto hizi tafuta msaada wa kitabibu,inaweza kuwa ni ishara ya uwepo wa matatizo ya afya.

Hatua nne za mzunguko wa tendo la ndoa zitakujia hapa hapa.

#Jifunzeuelimike
#KwahisaniyaAfyainfo
20190826_170325.jpeg
 
#KwahisaniyaAfyainfoView attachment 1190523
Hawa ndio wale wanaoomba kupumzika bila shaka...
 
Back
Top Bottom