Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limemkamata Mkazi wa Ichenjezya Wilayani Mbozi kwa tuhuma za kumbaka Mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 15.
RPC wa Songwe, Theopista Mallya amesema Baba huyo alitaka kufanya tukio hilo usiku wa manane ambapo aliingia kwenye chumba anacholala Mtoto huyo ndipo Mtoto huyo alipopiga kelele na Mama yake aliposikia na kufika akamkuta Mumewe anatoka chumbani kwa Mtoto wao.
"Baada ya kuingia chumbani Mtoto alimwambia anaumwa lakini yeye akamlazimisha ndipo Mtoto alipiga kelele mpaka Mama yake alipotoka chumbani na kwenda chumba cha Mtoto huyo"
"Baada ya Mtoto huyo kuhojiwa amesema Baba huyo ambaye ni Mlinzi katika moja ya Shule amekuwa akimfanyia kitendo hicho Mtoto huyo mara kwa mara wakati akimpelekea chakula kwenye lindo"
RPC amesema taratibu za kumfikisha Baba huyo kwenye vyombo vya sheria zinaendelea huku akitoa wito kwa Watu wenye tabia za kufanya vitendo hivyo kuacha mara moja.