Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jimbo la Momba, mkoani Songwe kimeeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya vitendo visivyofaa kwenye zoezi la uchaguzi ulioanza mapema leo, Jumatano Novemba 27.2024 ikiwemo baadhi ya wagombea wao kutokuta majina kwenye vituo vyao na kuongezwa vituo vya kupigia kura
Katibu wa CHADEMA jimbo la Momba Vicent Siame amesema ni masikitiko kuona serikali ikiweka mazingira magumu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji kwani baadhi ya wagombea wa CHADEMA wamewekewa ugumu kwa kukuta majina yao yamepelekwa vituo vingine hivyo kueleza kutokuwa na imani na wasimamizi wa uchaguzi huo katika jimbo lake na kutangaza kujitoa rasmi.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
"Pamoja na haya pia wameongeza vituo vya kupigia kura zaidi ya ishirini katika jimbo letu (Momba), huu ni uchafuzi sio uchaguzi bora tujitoe aibu zibaki kwao na naomba sana tuendelee na mapambano hata bila kushiriki uchaguzi"
Kwa upande wake kada wa CHADEMa Fanuel Siyame amedai kuwa hizo ni njama za CCM na serikali kuwapitisha wagombea wa CCM bila kupingwa na kueleza kuunga mkono mapendekezo na maazimio ya CHADEMA jimboni humo ya kususia uchaguzi huo
Siyame amesema katika maeneo mengi aliyozunguka amekuta kutokuwepo kwa majina ya wagombea kwenye karatasi/orodha ya wagombea badala yake majina yamepelekwa vituo vingine ikiwemo kitongoji cha Manda C na Chikamba kijiji cha Msangano, pia baadhi ya mawakala wametolewa nje ya vituo wakati waliapishwa
Baadhi ya wagombea waliodai kubadilishiwa vituo ni Alberto Siyame anayegombea kitongoji cha Chikamba, Adonia Medson Silungwe aliyekuwa akigombea kitongoji cha Mlanda C na jina lake amedai limeonekana kwenye kitongoji kingine cha Chikamba pamoja na Gabliel Siwila aliyekuwa akiwania nafasi ya mwenyekiti kitongoji cha Mlanda D
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Momba Fabian Manoza amesema zoezi la uchaguzi limeanza vizuri asubuhi ya Novemba 27, 2024 bila changamoto yoyote na kwamba kuhusu mawakala kudaiwa kutolewa nje ya vituo huenda ni kukosa sifa kwani walipewa maelekezo yote
Hata hivyo msimamizi huyo ambaye ndiye Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Momba amewaasa wananchi kupiga kura bila wasiwasi wowote kwa madai kuwa miundombinu yote iko vizuri na