Pre GE2025 Songwe: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Pre GE2025 Songwe: CV za Wabunge mwaka 2020 - 2025. Mbunge wako ametimiza ahadi zake?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wakuu,

1. George Ranwell Mwenisongole - Mbunge wa Songwe

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Aliibuka mshindi kwa kura 40,834, akimshinda mpinzani wake Pascal Yohana Haonga kutoka CHADEMA, aliyejikusanyia kura 18,054.

Elimu na Taaluma:

Elimu ya Msingi: Mbuyuni Primary School (1985 - 1991)

Elimu ya Sekondari: Jitegemee Secondary School (1992 - 1995) na Tambaza High School (1991 - 1999)

Elimu ya Juu: Alisoma katika Lincoln College na University of Central Arkansas, Marekani, ambapo alipata maarifa katika nyanja za biashara na usimamizi.

Kazi na Shughuli za Kisiasa:

Mwenisongole amekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya CCM, akiwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Kitaifa, Baraza la Utendaji la Mkoa, na Kamati ya Siasa ya Wilaya.

Uzoefu wa Kitaaluma: Alifanya kazi na Regional Bank USA kuanzia mwaka 2004 hadi 2010, na alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Geramo Enterprises (2013 - 2020).

2. Condester Michael Sichalwe - Mbunge wa Momba

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda uchaguzi kwa kupata kura 31,956, akimshinda Pascal Yohana Haonga kutoka CHADEMA aliyejikusanyia kura 19,771.

Elimu na Taaluma:

Elimu ya Msingi: Shule ya Maporomoko Primary School (1996), na alihitimu CPE katika Iyendwe Primary School mwaka 2002.

Elimu ya Sekondari: Mbeya Secondary School na Sangu Secondary School.

Elimu ya Juu: Alijiunga na Institute of Accountancy Arusha (IAA) mwaka 2010, ambapo alihitimu Shahada ya Uhasibu na Shahada ya Uzamili (2023).

Kazi na Shughuli za Kisiasa:

Sichalwe alifanya kazi kama Technician katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Computing Centre (UCC) mwaka 2009, na Field Technician katika IAA mwaka 2011.

Kati ya mwaka 2012 na 2013, alifanya kazi kama Software Programmer na IT Consultant katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (UNICTR).

Pia, alifanya kazi kama IT Consultant katika Arusha International Conference Centre (AICC).

Kwa sasa, ni Manager katika kampuni ya Forever Living, na alikuwa Diamond Coach wa Longrich Comp Ltd tangu 2018.

Safari ya Kisiasa: Alianza kujihusisha na siasa tangu mwaka 2000, akiwa chipukizi wa UVCCM.


3. David Silinde - Mbunge wa Tunduma

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2020: Alishinda kwa kupata kura 43,276, akimshinda Frank George Mwakajoka kutoka CHADEMA aliyejikusanyia kura 12,433.

Elimu:

Elimu ya Msingi: Shule ya Msingi Kilwa Masoko na Rungwa Primary School, Tanzania.
Elimu ya Sekondari: St. Mary’s Seminary na Minaki High School.
Elimu ya Juu: Bachelor’s Degree kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kazi na Shughuli za Kisiasa:

Aliingia bungeni mwaka 2010 kupitia CCM.

Aliteuliwa na Rais Magufuli kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

4. Japhet Ngailonga Hasunga - Mbunge wa Vwawa

Chama Cha Siasa: Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Matokeo ya Uchaguzi wa 2015: Aliibuka mshindi kwa kura 36,775 dhidi ya mpinzani wake.

Elimu:

Elimu ya Msingi: Shule ya Msingi Iyula (1976 - 1982).

Elimu ya Sekondari: Sangu Secondary School (1983 - 1986) na Mzumbe Secondary School (1987 - 1989), ambapo alihitimu CSEE na ACSEE.

Elimu ya Juu: Shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili (MBA).

Kazi na Shughuli za Kisiasa:

Alijiunga na CCM mwaka 2001 baada ya kuondoka NCCR-Mageuzi.

Alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2017, na baadaye alihudumu kama Naibu Waziri wa Kilimo.

Ana uzoefu mkubwa katika usimamizi wa fedha, elimu, utafiti, na katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii.
 
Labda neno sahihi ni wabunge wa ccm na si wabunge wetu
 
Hizi CV zina makosa

Moja, zinaonesha Haonga (Chadema), aligombea majimbo mawili kwa wakati mmoja.

PIli, David Silinde aliingia bungeni 2020, kama mbunge wa Chadema na sio CCM kama ilivyoandikwa.
 
Japheth hasunga alitokaje sangu akaenda mzumbe?
 
Back
Top Bottom