JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa utoaji wa Mikopo ya Asilimia Kumi kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na wenye Ulemavu iliyofanyika katika ukumbi wa Community Center uliopo wilayani hapo, Novemba 20, 2024, DC Mgomi amevipongeza vikundi vya maendeleo vilivyopata mkopo huo sambamba na kuvihimiza kuwekeza katika shughuli lengwa ili kupata faida pamoja na kurudisha marejesho ya mkopo huo.
DC Mgomi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kujali masilahi ya wananchi wa Wilaya ya Ileje kupitia mikopo hiyo inayolenga kuimarisha hali ya kiuchumi ya vikundi vya maendeleo.
Aidha, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya yetu, Nuru Waziri Kindamba kwa kusimamia na kuhakikisha zoezi la utoaji wa mikopo linakwenda vizuri.