KERO Songwe, Hospitali ya Mkoa boresheni idara zenu hasa Idara ya Macho

KERO Songwe, Hospitali ya Mkoa boresheni idara zenu hasa Idara ya Macho

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Twayemba

Member
Joined
Jan 29, 2024
Posts
12
Reaction score
14
Mfano mzuri wa changamoto ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe ni Idara ya Macho ambayo kiukweli haina utulivu kabisa. Mgonjwa anaambiwa aje Saa 2:00 Asubuhi kwa ajili ya operation, analazimika kusubiri kwa zaidi ya Saa 6 huku akiwa hajui kinachoendelea.

Akiingia chumba cha upasuaji, kelele za daktari zinaanza. Mara tuliza macho, mara hutoi ushirikiano. Kwani hivi hakuna vifaa na dawa za ganzi maalum ili jicho litulie? Jicho halitulizwi kwa kukemewa, bali kwa dawa.

Tunajua hospitali yetu ni changa na labda vifaa havitoshelezi sasa kama ni hivyo kulikuwa na ulazima wa kuanzisha idara bila kijipanga?

Kama sio dhambi, hawa Watumishi wapelekwe hata pale CCBRT ili wajifunze utendaji kazi wa Idara ya Macho unavyyofanyika.
Songwe2.png

Songwe11.png

Songwe.png
 
Sio huko tu asilimia kubwa hospital za serikali huduma ni mbovu
 
Back
Top Bottom