Pre GE2025 Songwe: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Pre GE2025 Songwe: Matukio Yanayojiri Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkoa wa Songwe ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania yenye postikodi namba 54100 ukiwa umemegwa kutoka ule wa Mbeya mwaka 2016.

Jina la mkoa limetokana na lile la mto Songwe. Makao makuu yako Vwawa.

Njombe.jpg

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa idadi ya watu katika Mkoa wa Songwe ni watu 1,344,687; wanaume 643,679 na wanawake 701,008.

Mkoa wa Songwe una majimbo sita (6) ya uchaguzi ambapo Jimbo la Mbozi linaongoza kwa kuwa na watu wengi (269,896) likifuatiwa na Jimbo la Momba (watu 259,781). Jimbo lenye idadi ndogo ya watu ni Jimbo la Ileje ambalo lina watu 125,869.

Orodha ya majimbo pamoja na mchanganuo wa idadi ya watu

Jimbo la Momba

  • Jumla ya watu 259,781 ambapo Wanaume ni 124,524 na Wanawake 135,257
Jimbo la Tunduma
  • Jumla ya watu 219,309, ambapo Wanaume ni 104,342 na Wanawake 114,967
Jimbo la Songwe
  • Jumla ya watu 229,129 , ambapo Wanaume ni 114,020 na Wanawake 115,109
Jimbo la Vwawa
  • Jumla ya watu 240,703, ambapo Wanaume ni 113,843 na Wanawake 126,860
Jimbo la Mbozi
  • Jumla ya watu 269,896, ambapo Wanaume ni 127,793 na Wanawake 142,103
Jimbo la Ileje
  • Jumla ya watu 125,869, ambapo Wanaume ni 59,157 na Wanawake 66,712
Soma Pia:
Hali ya Kisiasa

Ni kweli kwamba uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 nchini Tanzania ulileta mjadala mkubwa, hususan kuhusu hali ya demokrasia na nafasi ya vyama vya upinzani. Mkoa wa Songwe, kama ulivyoainisha, ulikuwa na majimbo yote sita yakichukuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), huku baadhi ya wagombea wakipita bila kupingwa.

Katika jimbo la Ileje, Eng. Msongwe Godfrey Kasekenya alitangazwa mshindi bila kupingwa.

Songwe - MULOGO PHILIPO AUGUSTINO naye alipita bila kupingwa

Katika majimbo kama Vwawa na Tunduma, kulikuwa na tofauti kubwa ya kura kati ya wagombea wa CCM na wale wa upinzani.

Vwawa

Japhet Hasunga (CCM) - Kura 38,226
Fanuel Mkisi (CHADEMA) - Kura 17,157

Tunduma -
David Silinde (CCM) - Kura 43,276
Frank Mwakajoka (CCM) - kura 12,433

Matukio kuelekea uchaguzi mkuu 2025

JANUARY

FEBRUARI
MACHI
 
Back
Top Bottom